RIVALDO AWEKA REKODI YA KUCHEZA TIMU MOJA NA MWANAE
Gwiji la soka nchini Brazil Rivaldo
ametengeneza historia baada ya kucheza timu moja na mtoto wake kwenye dimba
lililopewa jina la baba yake mzazi.
Rivaldo mwenye umri wa miaka 41, aliingia
kuchukua nafasi ya Mogi Mirim kwenye mchezo ambao ulimalizika kwa sare ya bao
1-1 kwenye mchezo wa ligi ya jimbo la Sao Paolo,mchezo huo ulichezwa kwenye dimba
la Romildo Ferreira.
Ilikuwa ni mara ya kwanza Rivaldo
kucheza mchezo wa ligi kwenye timu moja na mwanae Rivaldo Junior mwenye umri wa
miaka 18.
Mnamo mwaka 1996, mshambuliaji wa
zamani wa Chelsea na Barcelona Eidur Gudjohnsen aliingia uwanjani kuchukua
nafasi ya baba yake Arnor kwenye mchezo
wa timu ya taifa ya Iceland dhidi ya Estonia,kwahiyo ndoto yao ya kucheza pamoja
haikufanikiwa.
Category: uingereza
0 comments