Ratiba ya mechi zote za ligi kuu ya Tanzania bara wikiendi hii, hii hapa
Ligi
kuu ya Vodacom inaingia mzunguko wa 19 jumamosi hii kwa mechi tano,
zitakazochezwa katika miji ya Dar es Salaam, Bukoba, Morogoro, Tanga na
Arusha.
Mabingwa watetezi Yanga watakuwa nyumbani uwanja wa Taifa mjini Dar
es Salaam kumenyana na Ruvu Shooting ya mkoani Pwani, Nayo Kagera Sugar
ya Kaskazini magharibi mwa nchi hiyo inaikaribisha Rhino Rangers ya
Tabora katika mchezo utakaofanyika Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.Mjini Morogoro kutakuwa na mpambano kati ya Mtibwa Sugar na Ashanti United, wakati Coastal Union ya Tanga itaumana na timu ngeni na ngumu katika ligi hiyo-Mbeya City katika mechi itakayopigwa uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.
Kikosi cha maaskari jeshi wa Oljoro JKT watakuwa nyumbani kupambana na Askari wenzao Mgambo Shooting katika mchezo utakaofanyika kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Kaluta mjini Arusha.
Jumapili hii itakuwa zamu ya mabingwa wa Zamani wa ligi hiyo, Simba watakaoumana na JKT Ruvu, mchezo utakaochezwa Uwanja wa Taifa Dar es Salaam, huku Mechi kati ya Azam Fc na Tanzania Prisons ikichezwa kwenye uwanja wa Azam Complex Chamazi
Category: tanzania
0 comments