MESSI KWELI MKALI LAKINI SI ENGLAND...HAJAWAHI KUFUNGA BAO TANGU AMEANZA KUCHEZA

Unknown | 11:01 PM | 0 comments

MAKALI yake ya kufunga mabao yamemfanya awe na rekodi ya kipekee nchini Hispania – lakini huwezi amini Lionel Messi hajawahi kufunga mabo katika Uwanja wowote wa Ligi Kuu ya England.
Katika mechi nane alizocheza tangu mwaka 2006 kwenye viwanja vya Stamford Bridge, Anfield, Old Trafford na Emirates, nyota huyo wa Argentina hajaweza kutikisa nyavu popote.
Usiku wa leo kwenye Uwanja wa Etihad, Messi atakuwa anajaribu kuvunja rekodi yake ya kucheza dakika 717 bila kufunga bao.
Patupu: Katika saa 12 za kucheza kwenye viwanja vya timu kubwa England, Lionel Messi hajaweza kuifungia bao Barcelona
No hiding place: Messi makes his first appearance at the City of Manchester Stadium on Tuesday night and will be bidding to end his eight-game barren spell
Messi atacheza mechi ya kwanza kwenye Uwanja wa Man City usiku wa leo

REKODI YA MESSI VIWANJA VYA LIGI KUU ENGLAND

2006: 16 Bora- Chelsea 1-2 Barca ilishinda
2006: Makundi– Chelsea 1-0 Barca ilifungwa
2007: 16 Bora – Liverpool 0-1 Barca ilishinda
2008: Robo Fainali – Man Utd 1-0 Barca ilifungwa
2009: Nusu Fainali – Chelsea 1-1 Barca ilitoa sare
2010: Kufuzu – Arsenal 2-2 Barca ilitoa sare
2011: 16 Bora – Arsenal 2-1 Barca ilifungwa
2012: Nusu Fainali – Chelsea 1-0 Barca ilifungwa

Share story hii kupitia>>>>>> :
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

Category:

0 comments