MANCHESTER CITY vs CHELSEA KUONESHANA KAZI LEO, NI KOCHA YUPI MWENYE KIKOSI KAZI?

Unknown | 6:29 PM | 0 comments



Jose Mourinho kocha wa Chelsea na kocha wa Man City Manuel PellegriniJose Mourinho...........nimeipania sana City!!

Leo Jumatatu Usiku saa tano, Etihad, itazikutanisha Manchester City na Chelsea ambazo zinaifukuza Arsenal iliyo kileleni mwa Ligi Kuu England na umuhimu wa Mechi hii haujapotea kwa Jose Mourinho, Meneja wa Chelsea, ambae Siku zote yuko tayari kutumia mbinu yeyote ili kuzua hofu na kuwapoteza Wapinzani wake.

Safari hii, Mourinho ameipania Man City, ambao pamoja na Arsenal, ndio wanaonekana ni tishio kwake katika mbio za Ubingwa Msimu huu.Prolific: Alvaro Negredo has already scored 24 goals for Manchester City this season
Kwenye Mechi hii, Man City itamkosa Straika wao mahiri Sergio Aguero, ambae Msimu huu ameshafunga Bao 26, alieumia Musuli ya Pajani [Hamstring] walipoifunga Tottenham. 
Man City wameshinda Mechi zao zote 11 za Ligi walizocheza Uwanjani kwao Etihad Msimu huu wakipiga wastani wa Bao 4 kila Mechi na tayari washabamiza Jumla ya Mabao 115 katika Mechi zao zote za Msimu huu.

Share story hii kupitia>>>>>> :
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

Category:

0 comments