MANCHESTER CITY HIYOOOO ... YATINGA FAINALI YA CAPITAL ONE CUP.

Unknown | 8:12 AM | 0 comments


CITY_1_1273c.jpg
Timu ya Manchester City jana iliibuka na ushindi wa magoli 3-0 dhidi ya West Ham United katika mzunguko wa raundi ya pili ya kombe la ''Capita One Cup'' na hatimaye kujihakikishia kucheza fainali ya kombe hilo itakayofanyika March 2, 2014 katika uwanja wa Wembley, Manchester city inasubiri mshindi kati ya Manchester united au Sunderland ambao watacheza leo katika mzunguko wa pili wa ligi hiyo.
CITY_2_bfd87.jpg
Alvaro Negredo aliifungia Manchester City magoli mawili (2) wakati Sergio Arguero akimalizia goli la tatu na kuiwezesha Manchester City kuibuka na ushindi wa magoli 3-0, kwa matokeo hayo Manchester City iliibuka na ushindi kwa jumla ya magoli 9-0 kwa michezo yote miwili (Home and Away). Itakumbukwa kuwa Manchester City waliibuka na ushindi wa magoli 6-0 dhidi ya West Ham United katika uwanja wake wa nyumbani ''Etihad'' 
CITY_4_8b081.jpg
Manuel Pellegrini akuwachezesha wachezaji wake kama Yaya Toure, Vincent Company, Pablo Zabaleta, David Silva na wengine wakati timu hiyo ikichezesha wachezaji baadhi wanaowakilisha kikosi cha pili kama Boyata, Lescott,Lopes, Garcia na wengine, pia kuna baadhi ya wachezaji mahiri wanaowakilisha kikosi cha kwanza walitumika kuihakikishia Manchester City ushindi kama vile Fernandinho, Alvaro Negredo, Sergio Aguero, Nastasic, Clichy na Jesus Navas.
Mchezo ulikuwa na takwimu kama zinavyoonekana hapa chini.
CITY_3_d54e2.png
CITY_5_d7210.jpg
Manchester City itakutana na mshindi kati ya Manchester United au Sunderland mnamo tarehe 2, March/2014 katika uwanja wa Wembley ili kumpata mbabe wa kombe hilo la Capital One Cup.
Chanzo, skysports.com/uk

Share story hii kupitia>>>>>> :
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

Category:

0 comments