JE MANCHESTER UNITED WATARUDIA MAAJABU YA BLACKBURN ROVERS YA MWAKA 1995

Unknown | 12:12 AM | 0 comments

 




Msimu wa mwaka 1994/1995 katika ligi kuu nchini England Mabingwa walikua Blackburn Rovers chini ya Kenny Daglish.
Blackburn ndo timu pekee katika historia ya Ligi kuu England (EPL) ambayo ilichukua ubingwa huku ikiwa imefungwa mechi 7.
Mpaka sasa katika Ligi kuu England tumeshuhudia Man United ikipoteza mchezo wake wa 7 jana dhidi ya Chelsea katika mbio za kuchukua ubingwa. Swali ni Je wataweza kuvunja Rekodi ya Blackburn?
Mpaka ligi inashia msimu huo Blackburn ilikua imecheza mechi 42, Ikishinda 27, Ikitoka sare 8, Ilipoteza 7, Ilifunga magoli 80
na kufungwa magoli 39. 
Man United mpaka sasa imeshacheza mechi 22, Imeshinda 11, Imetoka sare 4, Imefungwa 7, Imefunga magoli 36 Imefungwa magoli 27.
JE DAVID MOYES NA KIKOSI KILICHOPO WANAWEZA?
By 
Mohd Khalifa Al-harth

Share story hii kupitia>>>>>> :
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

Category:

0 comments