BARCA NA MESSI WAO WAKWAMA KWA LEVANTE

Unknown | 10:16 AM | 0 comments


TIMU ya Barcelona imeacha pointi mbili mbele ya Levante baada ya sare ya kufungana bao 1-1 katika mechi ya La Liga usiku huu.
Vyntra alitangulia kuwafungia wenyeji dakika ya 10, lakini Gerard Pique akaisawazishia Barca dakika tisa baadaye. Lionel Messi alicheza lakini hakuweza kuziona nyavu za Levante zilizokuwa zinalindwa na kipa Keylor Navas aliyeokoa michomo mingi ya hatari.
Barca inaendelea kukaa kileleni kwa kutimiza pointi 51 baada ya kucheza mechi 20, sasa ikiizidi Real Madrid kwa pointi moja tu katika nafasi ya pili. Atletico Madrid inaweza kupanda kileleni ikiifunga Sevilla kwa kufikisha pointi 53, hadi sasa ikiwa inaongoza 1-0, bao la David Silva dakika ya 18 
Umetuokoa mwana: Gerard Pique akipongezwa na wachezaji wenzake, Alexis Sanchez na Lionel Messi baada ya kuisawazishia Barca

Share story hii kupitia>>>>>> :
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

Category:

0 comments