ZANZIBAR YAPUMULIA ‘MASHINE’ CHALLENGE, YAFUMULIWA 2-0 NA KENYA NAKURU

Unknown | 10:27 PM | 0 comments

Na Mahmoud Zubeiry, Nakuru
KENYA, Harembee Stars imeungana na Ethiopia kutinga Robo Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge baada ya kuifunga Zanzibar mabao 2-0 Uwanja wa Afrah, Nakuru jioni hii.
Mabao ya Harambee leo yamefungwa na beki wa Azam FC ya Dar es Salaam, Joackins Atudo kwa penalti dakika ya sita na mshambuliaji wa AFC Leopards ya Kenya, Allan Wanga dakika ya 60.
Beki wa Kenya, Joackins Atudo akipitia mpira miguuni mwa kiungo wa Zanzibar, Sabri Ali Makame leo Uwanja wa Afrah, Nakuru; na chini na wachezaji wa Harambee wakishangilia ushindi wao, wa kwanza kulia Allan Wanga aliyefunga bao la pili na wa pili kushoto ni Atudo aliyefunga la kwanza

Kwa ushindi huo, Kenya imetimiza pointi saba baada ya awali kuifunga Sudan Kusini 3-1 na kutoa sare ya bila kufungana na Ethiopia.
Zanzibar ambayo sasa inabaki na pointi zake tatu, itatazama mustakabali wake wa kwenda Robo Fainali katika nafasi mbili za best losers.
Rwanda ambayo haina pointi hadi sasa inaweza kuungana na timu moja ya kundi B pamoja na Zanzibar kuwania kufuzu katika nafasi za best losers, iwapo itaifunga Eritrea katika mchezo wake wa mwisho. 
Zambia, Tanzania Bara na Burundi timu mbili kati ya hizo zitafuzu moja kwa moja baada ya matokeo ya mechi za mwisho kesho na moja itaingia kwenye kapu la best losers.
Kundi C Uganda na Sudan tayari zimefuzu na Rwanda na Eritrea zitawania nafasi ya best losers. 
credit: Bin Zubeiry

Share story hii kupitia>>>>>> :
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

Category:

0 comments