ZAMBIA, SUDAN ZAIFUATA STARS NUSU FAINALI CHALLENGE

Unknown | 9:50 PM | 0 comments



Na Mahmoud Zubeiry, Mombasa
SUDAN imekamilisha orodha ya timu nne za kucheza Nusu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge mwaka huu baada ya kuitoa Ethiopia, kwa kuifunga bao 1-0 kwenye Uwanja wa County ya Mombasa, zamani Manispaa, Mombasa. 
Bao hilo pekee lilitiwa kimiani na Nadir Eltayeb dakika ya 23 kwa shuti la umbali, baada ya kumchungulia kipa wa Ethiopia, Derete Alemu.
Kundi A litakuwa na timu mbili Nusu Fainali, Zambia na Tanzania Bara

Kwa ushindi huo, Sudan imeungana na Tanzania Bara, Kenya na Zambia katika hatua hiyo, itakayochezwa katika miji miwili tofauti, Mombasa na Machakos. 
Katika mchezo wa kwanza, Zambia iliitoa Burundi kwa penalti 4-3, baada ya sare 0-0.
Nusu Fainali zote zitachezwa Jumanne, Tanzania Bara na wenyeji Kenya, Uwanja wa Kenyatta, Machakos na Sudan na Zambia Uwanja wa Manispaa, Mombasa.
Ikumbukwe tayari mabingwa watetezi, Uganda, The Cranes wamekwishatolewa na Tanzania Bara katika Robo Fainali ya Kwanza kabisa jana.    

Share story hii kupitia>>>>>> :
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

Category:

0 comments