YANGA SC KUANZA NA VIBONDE WA COMORO LIGI YA MABINGWA, AZAM FC NA FERROVIARIO KOMBE LA SHIRIKISHO

Unknown | 8:43 PM | 0 comments


Na Mahmoud Zubeiry wa Bin Zubeiry, Dar es Salaam
MABINGWA wa Tanzania, Yanga SC, watafungua dimba nyumbani na Komorozine ya Comoro katika Raundi ya Awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika, wakati Azam FC wataanzia nyumbani pia na Azam Ferroviario Da Beira ya Msumbiji katika Raundi ya Awali ya Kombe la Shirikisho.
Yanga wataanza na vibonde wa Comoro Ligi ya Mabingwa Afrika

Mechi za kwanza zitachezwa kati ya Febaruai 7, 8 na 9, wakati marudiano yatakuwa kati ya Februari 14, 15 na 16 February 2014. 
Azam wakifanikiwa kuitoa Ferroviario watamenyana na mshindi kati ya St. Michel ya Shelisheli na ASSM Elgeco Plus ya Madagacar.
Yanga wao, wakifuzu mtihani wao huo wa kwanza, watamenyana na mshindi kati ya Berekum Chelsea ya Ghana na Atlabar ya Sudan Kusini.
Azam na Ferroviarrio

Kwa mujibu wa droo iliyopangwa leo mjini Marrakech, Morocco, klabu 52 zitamenyana katika Raundi ya Awali ya michuano ya 18 ya Ligi ya Mabingwa mwakani kusaka nafasi za kuungana na mabingwa watetezi, Al Ahly ya Misri, Coton Sport ya Cameroon, TP Mazembe ya DRC, Hilal ya Sudan, CS Sfaxien na Esperance Sportive za Tunisia katika Raundi ya Kwanza.
Wawakilishi wa Zanzibar katika Shirikisho, Chuoni wataanzia nyumbani na How Mine ya Zimbabwe, wakati katika Ligi ya Mabingwa KMKM wataanzia ugenini na Dedebit ya Ethiopia.

Share story hii kupitia>>>>>> :
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

Category:

0 comments