WASANII KIBAO WAJITOKEZA KUSHIRIKI MKESHA WA MBIO ZA UHURU MARATHON
Katibu
wa kamati ya maandalizi ya mbio za uhurumarathon, Innocent Melleck,
akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar Es Salaam juu ya
maandalizi na wasanii watakaoshiriki kwenye mkesha wa Uhuru
utakaofanyika viwanja vya Leaders Club baada ya kukamilika kwa mbio za
uhuru. Kushoto ni katibu Mkuu wa Shirikisho la Riadha Tanzania Selemani
Nyambui.
*********************************
Na Mwandishi Wetu, Dar
ZIKIWA
zimebaki siku chache kwa ajili ya shindano la mbio ndefu za Uhuru,
'Uhuru Marathon', kufanyika, wasanii watakaotoa burudani siku ya mkesha
wa uhuru wapania kufanya kweli.
Wasanii
wanaotarajiwa kutoa burudani ni Roma Mkatoliki, Joh Makini, G Nako,
Nick wa Pili, Mrisho Mpoto, Mrisho Mpoto, TMK Wanaume, Mfalme Siboka na
kundi la Twanga Pepeta.
Wakizungumza
kwa nyakati tofauti, wasanii hao walisema wanashukuru kupewa heshima
kubwa kutumbuiza siku hiyo na hasa ukichukulia umuhimu wa amani, umoja
na mshikamano miongoni mwetu.
“Nitafanya
makamuzi ya kweli siku hiyo na watu wategemee mistari iliyokwenda
shule,” alisema Roma Mkatoliki, huku Mrisho Mpoto akidai ana vitu vikali
zaidi atakavyoweka hadharani siku hiyo.
Naye
Katibu wa Kamati ya Uhuru Marathon, Innocent Melleck alisema, homa ya
mbio hizo imepanda, hasa baada ya kujitokeza kwa wanariadha wengi wa
mataifa, kutoka nchi mbalimbali.
Melleck alisema, mbali na wengi kujitokeza bado anaamini wengi wataendelea kujiandikisha ili kufanikisha lengo la mbio hizo.
Aidha
alisema kuwa usajili bado unaendelea kwa wale wanaotaka kushiriki
ambapo fomu zitakazotolewa kwa mshiriki wa kilomita 3 atalipa Sh 100,000
yule wa kilomita 5 Sh 2,000 na washiriki wa kilomita 21 na 42 watalipia
Sh 6,000.
Category: tanzania
0 comments