TFF wataja hatua watakazochukua kwa Aden Rage

Unknown | 10:26 PM | 0 comments

 

MLIZNI
Rais wa TFF, Jamal Malinzi ameutolea ufafanuzi mgogoro wa Simba unaoendelea hivi sasa baada ya mwenyekiti wa Simba Ismail Aden rage kupinga agizo la kuitisha mkutano wa wanachama ndani ya siku 14 ambazo zinaisha Desemba 6. Malinzi ametaja hatua zitakazochukuliwa pale siku hizo zitakapoisha.
malinzi
‘tukizungumzia suala la klabu ya simba sports club ambae ni mwanachama wetu Tff,kama nilivyozungumza kwenye kikao chetu cha 23november Tff tulipokea barua mbili toka simba hapo nyuma,moja ilikua inatutaarifu kwamba kamati ya utendaji ya simba imemsimamisha mwenyekiti wake mheshimiwa Aden Rage,baadaye mwenyekiti wa Simba akatuandikia barua akasema hatambui kikao hicho,kwa hiyo kamati ya utendaji tulipokaa tukagundua kuna mgogoro baina ya mwenyekiti wa simba mheshimiwa Aden Rage  na kamati yake ya utendaji kwa hiyo tulichukua maamuzi kwa mujibu wa katiba yetu na kwa mujibu wa miongozo mbali mbali ya Caf na Fifa tukitambua simba ni mwanachama wetu kwa hiyo tukamuagiza mwenyekiti wa simba Aden Rage aitishe mkutano mkuu ukiwa na agenda moja ya kujadili mgogoro kati ya mwenyekiti na kamati yake ya utendaji’.
‘Huu ni utaratibu wa kawaida Fifa wanautumia dunia nzima,Caf wanautumia dunia nzima wanapoona kuna mahali hapajatulia,Tff haiwezi kuona nyumba inawaka moto ya mwanachama wake ikakaa kimya hilo halitotokea hata siku moja,tuna waachama 44 ambao ni vilabu vya premier ligi,vyama shiriki na vyama vya mkoa kuna wanachama 44 kwa hiyo kuna vyama vya mkoa 25,premier league ina wanachama 14 na vyama shiriki ni5 jumla 44′.
‘Tff ni yetu na siyo kuingilia katiba ya wanachama,Tff ni yetu siyo kuingilia maamuzi ya wanachama wetu lakini hatutokaa kimya pale tunapoona kuna tatizo,sasa leo ni tarehe 4 najua hatutoona tena hapa katikati kwa hiyo bora nilizungumzie liishe’.
‘Deadline ya maagizo ya Tff ni tarehe 6 december sasa maagizo haya hayakutolewa na Malinzi,mimi niliyatangaza kama msemaji mkuu wa Tff,maagiz toka tff kwenda klabu ya simba yalitolewa na kamati ya utendaji ya Tff,tarehe 22 itakua siku ya jumapili mwezi december kutakua na kikao cha kamatiu ya utendaji Tff,moja ya agenda za kikao hiki kitakua ni kujadili hali ilivyo ndani ya mwanachama wetu ambae ni Simba Sports Club,kwa hiyo vyovyote vile itakavyokua tarehe 6 vyovyote vile ambavyo ndo deadline ya maagizo ya Tff sekretarieti ya Tff  itatoa taarifa kwenye kamati ya utendaji ya Tff  ambayo itakaa tarehe 22 december na kamati ya utendaji ya Tff ndo ambayo itatoa maamuzi au maelekezo nini kifanyike’.
‘Niseme pia katika Agenda za kikao cha tarehe 22 december tutaunda vyombo vya kisheria vya Tff,tutaunda kamati ya rufaa,tutaunda kamati ya nidhamu,tutaunda kamati ya maadili,tutaunda kamati ya rufaa ya maadili,tutaunda kamati ya uchaguzi na tutaunda kamati ya rufaa ya uchaguzi’.
‘Siyazungumzii haya kwamba namtisha mtu la hasha,ni taarifa tu naitoa kwenu kwamba siku hiyo tutaunda hizi kamati ambazo zitaanza kutusaidia kuanzia siku hiyo kuweza kuongoza chombo chetu cha Tff kwa mujibu wa katiba yetu’.

Share story hii kupitia>>>>>> :
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

Category:

0 comments