SPURS YAZINDUKA, ADEBAYOR APIGA MAWILI WAKISHINDA 3-2 UGENINI, EVERTON YAICHINJA 2-1 SWANSEA NYUMBANI!!

Unknown | 11:06 PM | 0 comments

Goal! Adebayor stretched to reach Soldado's cross and poked it home

Na Baraka Mpenja kwa msaada wa Sportsmail
Tel: 0712461976 au 0764302956
MTU aliyesahaulika,  Emmanuel Adebayor amepiga mabao mawili katika ushindi wa 3-2 dhidi ya Southampton na kuongeza matumaini ya kocha wa muda wa Tottenham Hospurs Tim Sherwood kupata kazi ya kudumu.
Southampton wakiwa nyumbani walikuwa wa kwanza kutikisha nyavu za Spurs katika dakika ya 13 kupitia kwa Adam Lallana, lakini dakika ya 25, mshambuliaji nyota wa Spurs raia wa Togo, Emmanuel Adebayor aliisawazishia timu yake bao hilo.
Mpaka dakika 45 zinamalizika, ubao wa matangazo ulikuwa unasomeka 1-1.
Kipindi cha pili Spurs walikuja juu ya katika dakika ya  54, Jos Hooiveld alifunga bao la pili, lakini halikudumu kwani dakika tano tu baadaye, Rickie Lambert aliisawazisha bao hilo.

Dakika ya 64, Adebayor aliwainua vitini mashabiki wa Spurs baada ya kufunga bao la tatu na la ushindi.
Spurs waliingia uwanjani wakiwa na kumbukumbu ya kula kisago cha mabao 5-0 jumapili iliyopita kutoka kwa Liverpool  na kusababisha kocha mkuu Andre Villas-Boas kuoneshwa mlango wa kutokea kabla ya saa 24 kutimia tangu ale kipongo hicho.
Sherwood,  aliyekuwa Mkurugenzi wa maendeleo ya mpira wa klabu ya Tottenham alikabidhiwa majukumu ya kuongoza kikosi hicho. Alifungwa katika kombe la ligi `Capital One` na West Ham katikati ya wiki, na leo hii Adebayor amempa matumaini baada ya kuongoza timu katika ushindi wa 3-2 ugenini dimba la St Mary.
Detemined: Emmanuel Adebayor stares down some Southampton fans after putting Spurs level
Mkali wa kufumania nyavu: Emmanuel Adebayor aliwapunguza kasi mashabiki wa Southampton baada ya kuisawazishia bao la kwanza Spurs
Goal! Adebayor stretched to reach Soldado's cross and poked it home
Goooooo! Adebayor akifunga bao matata baada ya kupokea pande kutoka kwa Soldado

Delight: Sherwood punches the air as Spurs score their first goal, but insists he doesn't want to be a quick fix
Afadhali: Sherwood akishangilia bao lao la kwanza, lakini hataki kuwa mtu wa muda mfupi 
Moves: Referee Chris Foy looks on in wonderment as Adebayor dances in front of him
Kama maagizo vile!:  Mwamuzi, Chris Foy akimtazama Adebayor aliyekuwa akicheza mbele yake baada ya kufunga
Kikosi cha Southampton: Gazzaniga 6, Chambers 7, Hooiveld 5, Lovren 6, Fox 5 (Gallagher  78 min); Schneiderlin 6, Davis 6 (Ramirez 69, 5), Cork 6 (Ward-Prowse 63, 6); Lallana 8, Lambert 6, Rodriguez 5.
Kikosi cha Spurs: Lloris 6; Walker 7, Dawson 7, Chiriches 6, Rose 6; Lamela 5 (Chadli 60, 7), Eriksen 6, Dembele 5 (Bentaleb 50, 7), Sigurdsson 6; Adebayor 8, Soldado 6 (Defoe 85).
Opener: Adam Lallana celebrates after putting Southampton ahead on 13 minutes
Bao la kuongoza: Adam Lallana akishangilia baada ya kufunga bao la kuongoza kwa Southampton katika dakika ya 13
Bunduki: Lallana akipiga shuti umbali wa mita 25  na kuandika bao kimiani
Katika mchezo mwingine, Swansea City wakiwa nyumbani wamefungwa mabao 2-1 dhidi ya Everton.
Everton walikuwa wa kwanza kuliona lango la wenyeji wao katika dakika ya 66 kupitia kwa Seamus Coleman akipokea pasi kutoka kwa James McCarthy.
Bryan Oviedo katika dakika ya 70 aliisawazishia Swansea bao hilo, lakini jahazi lao likazama dakika ya  84′ kupitia kwa Ross Barkley

Share story hii kupitia>>>>>> :
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

Category:

0 comments