PETER MANYIKA AVAA MEDALI YA KWANZA NCHINI OMAN
Golikipa wa zamani wa vilabu vya Sigara,Yanga na Mtibwa Sugar pamoja na Taifa Stars Peter Manyika amefanikiwa kuvaa medali ya mshindi wa pili ya kombe la chama cha soka nchini Omani.
Manyika ambaye kwasasa ni kocha wa makipa wa timu ya SEEB CLUB,aliiongoza timu yake kupoteza mchezo wa fainali mbele ya timu ya SUR CLUB kwa mikwaju ya penati 3-2 baada ya timu hizo kumaliza dakika 90 bila kufungana.
Category: tanzania
0 comments