MOURINHO AKIRI `HAKUNAGA` KAMA AGUERO AU SUAREZ, AWAPA MAKAVU `LAIVU` BA, ETO`O, TORRES!!
Na Baraka Mpenja kwa msaada wa Sporstmail
Tel: 0712461976 au 0764302956
KOCHA Jose Mourinho amekiri kuwa
washambuliaji wake Demba Ba na Fernando Torres hawana kiwango bora kama
Sergio Aguero au Luis Suarez.
Bosi huyo wa Chelsea alisema:
‘Baadhi ya washambuliaji wanacheza kwa kiwango cha juu na wanaonesha
vipaji binafsi na wanaweza kufanya kile ambacho timu zao haziwezi
kufanya. Washambuliaji wetu hawana ubora kama huu au umuhimu`..
‘Siwakosoi hawa jamaa kwasababu
wanafanya kazi nyingine. Uwezo wao wa kufunga ni mdogo na unawaumiza
kicha wao na mimi pia, lakini mchango wao kwa timu ni mzuri`.
Hawana lolote?: Jose Mourinho hafurahishwi na kiwango cha washambuliaji wake watatu
Washambuliaji watatu wa Chelsea, Torres, Ba, Eto`o wameshindwa kumfurahisha kocha wao Jose Mourinho
Mreno
huyo alikatishwa sana tamaa na washambuliaji wake baada ya kupoteza
nafasi nyingi katika mchezo wa ligi kuu waliolala bao 3-2 dhidi ya Stoke
City.
‘Washambuliaji
wengine(Aguero na Suarez) wanacheza kwa nguvu na kuonesha kiwango
binafsi, wanapiga chenga, wanapiga mashuti langoni, wapo imara na
wanaendana na kasi ya mpira. wanatatua matatizo kiukweli`. Alisema
Mourinho.
`Hatuna washambuliaji wa aina hii na nataka wafanye kazi tofauti na sasa`.
“Nahitaji
zaidi?, ndiyo. Tunataka zaidi?, ndiyo. Lakini tusitarajie Demba au
Fernando kucheza soka kama Sergio Aguero au Luis Suarez, kupiga chenga
na kufunga kwa ubora” Alisema Mourinho.’
Anaogopa nyavu nini?: Jose Mourinho akimuangalia Fernando Torres wakati wa mazoezi uwanja wa Cobham
Category: uingereza
0 comments