Mechi ya Kilimanjaro Stars na Harambee Stars yasogezwa mbele.

Unknown | 8:09 PM | 0 comments

     
Tanzania-celebrate-1-300
Mchezo wa nusu fainali ya michuano ya GOTV SENIOR CECAFA CHALLENGE CUP unaozikutanisha timu mwenyeji The Harambee Stars ambayo ni timu ya taifa ya Kenya na Tanzania The Kilimanjaro Stars uliokuwa uchezwe kwenye uwanja wa Kenyatta huko Machakos saa 10 jioni kwa muda wa Afrika mashariki umesogezwa mbele baada ya mvua kubwa iliyonyesha kwenye uwanja huo kufanya mazingira ya mchezo kuendelea kuwa magumu.
Mchezo huo umelazimika kuhamishwa toka kwenye uwanja huo wa machakos hadi uwanja wa nyayo Nairobi ambapo sasa utapigwa saa 12 jioni .
Nusu fainali nyingine kati ya Zambia na Sudan inatarajia kuanza dakika chache zijazo kwenye uwanja wa Manisapaa huko Mombasa.

Share story hii kupitia>>>>>> :
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

Category:

0 comments