MAN CITY YAMKALISHA BINGWA WA ULAYA NYUMBANI KWAKE, YATOKA NYUMA KWA 2-0 NA KUSHINDA 3-2

Unknown | 9:06 AM | 0 comments

 

KLABU ya Manchester City imewafunga mabingwa wa Ulaya Bayern Munich mabao 3-2 Uwanja wa Allianz Arena, Munich katika mchezo wa Kundi D, Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Thomas Muller alitangulia kuwafungia wenyeji bao dakika ya tano, pasi ya , Dante na Mario Gotze akafunga lpili dakika ya 12, kabla ya City kuanza safari ya kupanda mlima hadi kuibuka na ushindi huo.
David Silva alifunga la kwanza dakika ya 28 pasi ya James Milner na Kolarov akafunga la kusawazisha dakika ya 59 kabla ya Milner kufunga la ushindi dakika ya 62, pasi ya Jesus Navas.
Kwa ushindi huo, City imetimiza pointi 15 sawa na Bayern baada ya kucheza mechi sita, lakini mabingwa wa Ulaya wanaendelea kukaa kileleni mwa Kundi D, kutokana na wastani wao mzuri wa mabao ya kufunga na kufungwa.
James Milner alifunga mabao mawili City ikiilaza 3-2 Bayern
Man City could have gone through with another goal, based on their head-to-head record against Bayern
Bayern inaendelea kuongoza Kundi D kwa wastani mzuri wa mabao
Mishap: Pellegrini brought off Edin Dzeko in the closing stages and brought on Jack Rodwell
Kocha Pellegrini alimtoa Edin Dzeko dakika za mwishoni

Share story hii kupitia>>>>>> :
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

Category:

0 comments