Liverpool yaifumua Tottenham Hotspurs 5-0.

Unknown | 11:25 PM | 0 comments

 

liverpool rout
Mashabiki wa klabu ya Iverpool hii leo walikuwa na raha ya aina yake baada ya kuishuhudia timu yao ikiifunga Tottenham Hotspurs bila huruma .
Liverpool walishinda mchezo uliopigwa kwenye uwanja wa nyumbani wa Tottenham kwa matokeo ya   5-0 hali ambayo iatzidi kukiweka shakani kibarua cha kocha Mreno wa Spurs Andre Villas Boas.
Wafungaji wa Liverpool kwenye mchezo huo walikuwa Luis Suarez ambaye alifunga mabao mawili na kufikisha idadi ya mabao 18 kwa msimu huu, Jordan Henderson , Raheem Sterling na John Flanagan .
spurs hit for 5
Tottenham walimaliza mchezo huo wakiwa pungufu baada ya kiungo Mbrazil Paulinho kuonyeshwa kadi nyekundu kwa kumchezea rafu Luis Suarez.
Ushindi huo unawarudisha Liverpool kwenye nafasi ya pili wakiwa wamefikisha pointi 33 ambapo wanawazidi Chelsea kwa tofauti ya mabao huku wakiwa nyuma ya Arsenal kwa pointi mbili pekee.

Share story hii kupitia>>>>>> :
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

Category:

0 comments