JAMAL MALINZI AKABIDHIWA RIPOTI NA KAMATI YA KANAL KIPINGU.

Unknown | 8:52 PM | 0 comments

 






Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania, TFF jana lilipokea ripoti maalum kutoka kwenye jopo la baadhi ya wataalam waliokutana hivi karibuni visiwani Zanzibar kwa ajili ya kutafuta mustakabali wa Tanzania kufuzu michuano ya AFCON 2015 itakayofanyika nchini Morocco.
Ripoti hiyo imewasilishwa kwa Rais wa TFF Jamali Malinzi na mwenyekiti wa jopo hilo Kanali Mstaafu Iddi Kipingu baada ya jopo hilo kukamilisha jukumu walilopewa.
Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo mwenyekiti wa jopo hilo Kanali Mstaafu Kipingu amesema kwamba kazi hiyo wameifanya kwa uzalendo na uadilifu mkubwa.

Share story hii kupitia>>>>>> :
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

Category:

0 comments