DILUNGA AANZA RASMI MAZOEZI YANGA
Unknown |
10:09 PM |
0
comments
KIUNGO
mpya wa Yanga, Hassan Dilunga leo asubuhi ameanza mazoezi katika klabu
yake mpya aliyojiunga nayo hivi karibuni akitokea Ruvu Shooting ya
Pwani.
Dilunga
alikuwa mchezaji wa pili kusajiliwa na Simba baada ya Yanga baada ya
Juma Kaseja ili kutimiza matakwa ya kocha Ernie Brandts ambaye aliwataka
wachezaji hao ili kuimarisha kikosi chake.
Kiungo
huyo aliwasili katika mazoezi hayo yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Bora,
Kijitonyama na kujiunga na wenzake walioanza mazoezi hayo wiki mbili
zilizopita.Dilunga alikuwa
sambamba na nyota wengine wa Yanga waliokuwa wakizitumikia timu zao za
taifa katika michuano ya Kombe la Chalenji iliyofanyika Kenya na
kumalizika wiki iliyopita huku wenyeji wakitwaa ubingwa.
Wachezaji
walioanza mazoezi leo sambamba na Dilunga ni Deo Munishi, Frank Domayo,
Athuman Idd ‘Chuji’ na Mrisho Ngassa ambao walikuwa wakiichezea timu ya
taifa ya Tanzania Bara maarufu kama Kilimanjaro Stars ambayo iliishia
robo fainali ya michuano hiyo.
Muda
mfupi baada ya mazoezi hayo, Dilunga alisema hawezi kuzungumza maneno
mengi kwa kuwa ndiyo kwanza amejiunga na timu hiyo hivyo aachwe hadi
atakapofanya mazoezi kwa siku kadhaa.
“Unajua
siwezi kusema lolote hapa kama unavyoona mimi nimeanza mazoezi leo sasa
hakuna ninalolijua katika timu lakini nikitulia kwa muda naweza kuwa na
jambo la kuongea,” alisema Dilunga.
Yanga
inafanya mazoezi kujiandaa na mechi yake dhidi ya Yanga itakayochezwa
Jumamosi ijayo kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ambayo imeandaliwa
na wadhamini wao Kampuni ya Bia Tanzania (TBL).
Pia
Yanga inajiandaa na mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Bara itakayoanza
Januari 25 mwakani. Maandalizi hayo ya Yanga pia yanahusu ushiriki wao
wao wa Ligi ya Mabingwa Afrika mwakani.
na Shaffihdauda Blog
Category: tanzania
0 comments