YANGA WAMALIZA MZUNGUKO WA KWANZA KWA KUTOA KIPIGO CHA 3-0 NA KUPANDA KILELENI, AZAM FC VS MBEYA CITY NGOMA NZITO CHAMAZI, RHINO VS PRISONS SULUHU

Unknown | 12:45 PM | 0 comments

 



IMG_0124

Na Baraka Mpenja wa Fullshangwe,  Dar es salaam

MABINGWA watetezi wa ligi kuu soKA Tanzania bara, Dar Young Africans wamefanikiwa kumaliza mzunguko wa kwanza ligi kuu msimu wa 2013/2014 wakiwa kileleni baada ya ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya JKT Oljoro ya Arusha, huku waliokuwa vinara, Azam fc wakilazimishwa sare ya 3-3 dhidi ya Mbeya City.

Yanga wamekwaa kileleni baada ya kufikisha pointi 29, huku Azam fc wakiwa wa pili kwa pointi 27, Mbeya City wa tatu wakijikusanyia pointi 27, na Mnyama Simba anabaki nafasi ya nne akiwa na pointi 24.


Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, mabao ya Yanga yalifungwa na Simon Msuva dakika 23, Mrisho Ngassa dakika ya 23 na Jerry Tegete dakika ya 53.

Huko  Azam Complex, Chamazi, hadi mapumziko, timu hizo zilikuwa zimekwishafungana bao 1-1, Azam wakitangulia kupata bao kupitia kwa Humphrey Mieno dakika ya 13 na Mbeya City wakasawazisha kupitia kwa Mwagane Yeya ‘dakika ya 30.

Kipindi cha pili dakika ya 52 Mbeya City waliandika bao la pili kupitia kwa Yule Yule mtambo wa kurekebisha mabao , Mwagane Yeya akiunganisha krosi iliyochongwa na Steven Mazanda, lakini John Bocco ‘Adebayor’ akaisawazishia Azam dakika ya 60 akiunganisha krosi ya Kipre Tchetche.

Mwagane aliifungia tena Mbeya City bao la tatu katika dakika ya 73 na kuwainua vitini mashabiki wao waliokuwepo Azam Complex,  lakini dakika ya 83 Khamis Mcha ‘Vialli’ aliisawazishia timu yake bao hilo.

goli azamPicha na Bin Zubiery

Azam; Mwadini Ally, Erasto Nyoni, Waziri Salum, Said Mourad, Aggrey Morris, Kipre Balou, Salum Abubakar, Kipre Tchetche, John Bocco/Joseph Kimwaga 72, Humphrey Mieno na Farid Mussa/Khamis Mcha dk80.
Mbeya City; David Burhan, John Kabanda, Hassan Mwasapili, Deogratius Julius, Yussuf Abdallah, Anthony Matogolo, Mwagane Yeya, Steven Mazanda/Alex Sethi dk90, Paul Nonga/Francis Castor, Deus Kaseke.

Huko Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora, Maafande wa jeshi la wananchi Tanzania (JWTZ) waliwakaribisha Tanzania Prisons ya Mbeya na timu hizo kuchoshana nguvu baada ya suluhu ya bila kufungana.

Share story hii kupitia>>>>>> :
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

Category:

0 comments