SIMBA SC YASAJILI VIFAA VIWILI HATARI VYA ZANZIBAR HEROES, MMOJA ALICHEZA LIGI KUU MISRI WATAZAME HAPA.

Unknown | 12:01 AM | 0 comments

Na Mahmoud Zubeiry, Samora
SIMBA SC imesajili wachezaji wawili kwa mpigo leo hii, kiungo mchezeshaji Awadh Juma Issa kutoka Mtibwa Sugar ya Morogoro na Ally Badru Ally kutoka Canal Suez ya Ligi Kuu ya Misri.
Wachezaji hao wawili wa timu ya soka ya taifa ya Zanzibar wamesaini adhuhuri ya leo, nyumbani kwa Mwenyekiti wa Simba SC, Alhaj Ismail Aden Rage, Mtaa wa Samora, Dar es Salaam.


Mwenyekiti wa Simba SC, Alhaj Rage (katikati) akiwa na Badru Ally kulia na Awadh Juma kushoto nyumbani kwake leo baada ya kuwasaini.

Walitua kwa ndege maalum na mchana wakaenda kusaini mikataba ya miaka miwili kila mmoja na baada ya hapo, wakarejea kwenye kambi ya Zanzibar Heroes inayojiandaa na michuano ya CECAFA Challenge.
Akizungumza baada ya kuwasajili wachezaji hao, Rage ambaye ni Mbunge wa jimbo la Tabora Mjini (CCM), alisema kwamba usajili huo umetokana na mapendekezo ya benchi la Ufundi.
“Ni wachezaji wazuri, ambao tunawajua vizuri na tumekuwa tukiwafuatilia kwa muda mrefu na tuna imani nao sana kwamba watakuja kuisaidia timu yetu,”alisema Rage.




Awadh Juma akitia dole gumba pembeni ya Alhaj Rage


Awadh Juma akiwa ameshika kwa pamoja na Rage Mkataba wake


Badru akisaini pembeni ya Alhaj Rage


Badru akiwa ameshika kwa pamoja na Rage Mkataba wake


Badru akisaini kurasa za Mkataba 


Msomi; Katibu Mkuu wa Simba SC, Evodius Mtawala akiupitia Mkataba aliouandaa kabla ya kuuchapisha ili wachezaji hao wasaini 
Kwa upande wake, Badru alisema kwamba amefurahi sana kusaini Simba SC na anaamini nyota yake itang’ara huko. “Simba SC ni timu kubwa, maarufu, naamini kabisa hapa nitafanya vizuri, kikubwa tu naomba sapoti ya mashabiki wote,”alisema.
Kuhusu klabu yake ya Misri aliyoichezea tangu mwaka 2010, Badru alisema kwamba imemruhusu kuondoka ingawa alikuwa ana miaka miwili zaidi katika Mkataba wake na klabu hiyo. 
Juma ambaye ameichezea Mtibwa Sugar kwa miaka miwili tangu alipojiunga nayo akitokea Taasisi ya Soka Tanzania (TSA) ambako alikuwa pamoja na Thomas Ulimwengu alisema kwamba amefurahi kutua Msimbazi.
“Nimefurahi sana kuja Simba SC, ni ndoto zangu za muda mrefu na sasa ni wakati wa kufanya kazi tu,”alisema


CREDIT: http://bongostaz.blogspot.com

Share story hii kupitia>>>>>> :
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

Category:

0 comments