MABINGWA WATETEZI WA CECAFA, UGANDA THE CRANES YAWALIZA RWANDA 1-0, KIIZA, NIYONZIMA NDANI, SUDAN YAJIPIGIA ERITREA 3-0
Na Baraka Mpenja wa Fullshangwe, Dar es salaam
MICHUANO
ya kombe la mataifa ya Afrika mashariki na kati, CECAFA Challenge
imeendelea leo hii kwa timu za kundi C kushuka dimbani kusaka pointi
tatu muhimu.
Mchezo
wa jioni uliwakutanisha mabingwa watetezi, korongo wa Kampala, timu ya
Taifa ya Uganda dhidi ya Rwanda, Amavubi na kushuhudia The Cranes
wakiibuka na ushindi wa bao 1-0 kwenye uwanja wa Nyayo , jijini Nairobi.
Katika
mchezo wa leo, shughuli ilikuwa pevu na ilisubiria dakika ya 88 ambapo
Uganda waliandika bao lao pekee kupitia kwa nyota wao Dan Sserunkuma .
Amavubi
walionesha kandanda safi na kutawala mchezo kwa kiasi kikubwa na kupata
nafasi za kufunga, lakini walishindwa kuzibadili kuwa mabao na
wakafanya kosa moja dakika za lala salama na kushuhudia Uganda
wakipachika gozi kimiana na kulaza mechi hiyo kwa ushindi huo wa kwanza
katika harakati zao za kuteta ubingwa wao.
Nyota
wa mabingwa watetezi wa ligi kuu soka Tanzania bara, Dar Young
Africans, Khamis Friday Kiiza `Diego wa Kampala` alicheza kwa upande wa
Uganda na mwenzake Haruna Hakizimana fadhili Niyonzima alionesha
maujanja yake katika kikosi chake cha Rwanda.
Mbali
na mchezo huo wa jioni, kuna mchezo wa kwanza ambao Sudan walishuka
dimbani kupepetana na Eritrea kwenye Uwanja wa Kenyatta, Machakos.
Katika
mchezo huo, Sudan waliibuka na ushindi mnono wa mabao 3-0. Mabao
yamefungwa na Salah Ibrahim akifunga mawili na Tahir Mohammed akijipigia
moja.
Mechi za leo zimekamilisha mechi za kwanza za makundi na mechi za pili zitaanza kesho.
Ethiopia
watakuwa kibaruani kuvaana na Mashujaa wa visiwani, Zanzibar Heroes,
wakati wenyeji Kenya watakabiliana na Sudan Kusini kwenye uwanja wa
Nyayo. Hizo zitakuwa mechi za kundi A.
Katika mechi za kwanza za kundi hilo, Zanzibar iliifunga Sudan Kusini 2-1 na Kenya ilitoka sare ya bila kufungana na Ethiopia.
Category: tanzania
0 comments