KILIMANJARO STARS YAAGWA LEO, WACHEZAJI WAAHIDI MAKUBWA
Wachezaaji wa Kilimanjaro stars |
Kikosi
cha Kilimanjaro Stars imeagwa leo tayari kwa safari ya Nairobi, Kenya
kushiriki michuano ya Kombe la Chalenji inayoanza kutimua vumbi Novemba
27 mwaka huu.
Hafla
ya kuiaga timu hiyo imefanyika saa 5 asubuhi kambini kwao katika hoteli
ya Accomondia jijini Dar es Salaam. Msafara wa Kilimanjaro Stars
inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager unaongozwa na Ahmed Idd
Mgoyi. Timu itaondoka saa 10 alasiri kwa ndege ya RwandAir.
Wachezaji waliomo katika msafara huo ni
makipa Deogratius Munishi (Yanga), Ivo Mapunda (Gor Mahia, Kenya) na
Aishi Manula (Azam). Mabeki ni Erasto Nyoni (Azam), Himid Mao (Azam),
Ismail Gambo (Azam), Kelvin Yondani (Yanga), Michael Pius (Ruvu
Shooting) na Said Moradi (Azam).
Viungo ni Amri Kiemba (Simba), Athuman
Idd (Yanga), Frank Domayo (Yanga), Haruna Chanongo (Simba), Hassan
Dilunga (Ruvu Shooting), Ramadhan Singano (Simba) na Salum Abubakar
(Azam).
Safu ya ushambuliaji inaundwa na Elias
Maguli (Ruvu Shooting), Faridi Musa (Azam), Joseph Kimwaga (Azam), Juma
Liuzio (Mtibwa Sugar), Mbwana Samata (TP Mazembe, DRC), Mrisho Ngasa
(Yanga) na Thomas Ulimwengu (TP Mazembe, DRC).
Hata hivyo, washambuliaji Samata na
Ulimwengu watajiunga na timu hiyo jijini Nairobi, Desemba Mosi mwaka huu
wakitokea Lubumbashi ambapo Novemba 30 mwaka huu TP Mazembe itacheza
fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika.
Benchi la Ufundi la timu hiyo
linawajumuisha Kim Poulsen (Kocha Mkuu), Sylvester Marsh (Kocha
Msaidizi), Juma Pondamali (Kocha wa Makipa), Leopold Tasso (Meneja wa
Timu), Dk Mwanandi Mwankemwa (Daktari wa Timu), Frank Mhonda (mtaalamu
wa tibamaungo) na Alfred Chimela (Mtunza Vifaa).
Kilimanjaro
Stars ambayo ipo kundi B katika michuano hiyo itacheza mechi yake ya
kwanza Novemba 28 mwaka dhidi ya Zambia kwenye Uwanja wa Machakos.
Category: tanzania
0 comments