HASSANOL ASHINDA KESI YA WIZI WA SHABA

Unknown | 5:06 PM | 0 comments

 

 

Hassan Hasanol akipelekwa kizimbani.
Wambura Mahenya (kushoto) akikumbatiwa na ndugu yake anayelia kwa furaha.
Ndugu na jamaa wakitoka nje ya mahakama.
Licha ya kushinda kesi, Hasanol akirudishwa lupango.
Aliyekuwa mshitakiwa namba mbili, Dokta Najim akiondoka kwa furaha.
 
Aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa timu ya Simba, Hassan Othman ‘Hasanol’ leo ameshinda kesi ya wizi wa shaba ya zaidi ya shilingi milioni 300, iliyokuwa ikimkabili kwenye mahakama ya Kisutu jijini Dar es Salaam. Katika kesi hiyo mshitakiwa wa pili alikuwa ni baba mkwe wa Hasanol aitwaye Dokta Najim Kisega na mshitakiwa wa tatu alikuwa Wambura Mahenya Kisiroti.  Baada ya hakimu, Sundi Fimbo kuwaachia huru wote watatu maafande wa Jeshi la Magereza waliendelea kumng'ang'ania Hasanol kwa kesi nyingine inayomkabili ya meno ya tembo.
(PICHA : RICHARD BUKOS / GPL)
 

Share story hii kupitia>>>>>> :
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

Category:

0 comments