DILUNGA AJIPIGA KITANZI YANGA CHA MIAKA 3
KIUNGO
Hasaan Saleh Dilunga katikati ya wiki hii alisaini mkataba wa miaka
mitatu kuitumikia klabu ya Young Africans akitokea timu ya Ruvu Shooting
aliyokua akiitumikia katika kipindi cha pili mfululizo katika Ligi Kuu
ya Vodacom.
Mapema
mtandao rasmi wa klabu uliandika juu ya taarifa za usajili wa kiungo
huyo kusaini mkataba wa miaka mitatu kuanzia mzunguko wa pili wa Ligi
Kuu na mashindano ya kimataifa ambayo timu ya Yanga itashiriki.
Kutua
kwa Dilunga katika klabu ya Young Africans kulizua maswali mengi huku
baadhi ya mitandao ikisema mchezaji huyo hajasajiliwa na mabingwa
watetezi wa Ligi Kuu ya Vodacom Yanga SC na kuwa mtandao wa klabu
umekurupuka.
Akiongea
na www.youngafricans.co.tz Afisa Habari wa Yanga Baraka Kizuguto
amesema Dilunga alikamilisha taratibu zote na kusaini mkataba na Yanga
kwa miaka mitatu mbele ya viongozi wa Yanga ambao pia walishamalizana na
uongozi wa Ruvu Shooting kabla ya kufikia kumsainisha mchezaji.
"Hatuna
taratibu za kuongopa wala kutoa taarifa zisizo na ukweli katika mtandao
wetu, mtandao wetu umekuwa maarufu ndani na nje ya nchi kwa sababu ya
kutoa habari za ukweli na zenye uhakika kwa hiyo hatukukurupa juu ya
hilo" alisema Kizuguto.
Aidha
aliongeza Ukitazama idadai ya watu wanaotembelea mtandao wetu ndani na
nje ya nchi achilia mbali facebook na twitter bado tumekua na watu wengi
sana ambao wameijua Yanga, wanaipenda Yanga, wanaifuatilia Yanga
kupitia mtandao wake wa klabu hivyo hatuwezi kuwaangusha kwa kutoa
taarifa za uongo.
Dilunga
alisaini mkataba wa kuitumikia Yanga katikati ya wiki mbele ya viongozi
wa kamati ya mashindano waliongozwa na Abdallah Bin Kleb, Mussa
Katabaro na Isaac Chanji. IMEHAMISHWA KUTOKA TOVUTI YA YANGA SC
Category: tanzania
0 comments