SIR ALEX FERGUSON AANIKA SIRI NZITO
Aliekua kocha wa club ya Manchester United Sir Alex Ferguson ambae hivi juzi jina lake lilizinduliwa rasmi kutumika kwenye moja ya barabara zilizokaribu na uwanja wa Old Traford, amekitambulisha kitabu chake kinaitwa ‘My Autobiography‘
Amezungumzia mambo kadhaa ndani ya hiki kitabu ikiwemo pia maisha yake ya soka kwa ujumla, vitu alivyokutana navyo.. wachezaji pamoja na matukio makubwa likiwemo la David Beckham kuondoka Manchester United mwaka 2003 ambapo namkariri akisema…
1. ‘Beckam alijiona yeye ni mkubwa kuliko Alex Ferguson, yani staa kuliko mimi’
2. Alipoingia mapenzini na Victoria ndio kila kitu kilibadilika kuhusu yeye.
3. ‘Mimi ni mtu wa soka, wakati alipoiacha Real Madrid na kwenda LA Galaxy, kama angeniomba maoni ningemwambia exactly nilichokua nacho moyoni’
4. ‘Siku ulipotokea mkwaruzano kati yangu na yeye baada ya 2-0 dhidi ya Arsenal ndio ulikua wakati wa mwisho wa David Beckham Manchester United, majibu ya Beckham kwangu ndio yalinikasirisha sana’
5. ‘Nilikataa mara mbili ofa ya kuwa kocha wa England’
Category: uingereza
0 comments