Simba mpya, Yanga ile ile, jumapili Taifa patachimbika!!

Unknown | 9:46 AM | 0 comments

 

puppies-cute-animal-hd-wallpaper
Kikosi cha Simba Sc
Dhaira, Owino, Tambwe, Kaze na Mwombeki ni miongoni mwa wachezaji wapya waliosajiliwa na Simba na ambao wamejihakikishia namba kwenye timu hiyo inayofundishwa na Kocha Abdalah Kibadeni na msaidizi wake, Jamhuri Kihwelo.
JOSEPH Owino amewaambia mastraika wa Simba kwamba yeye atakuwa makini sana kwenye ulinzi kuikabili Yanga na wao wapige mabao ya haraka haraka.
Lakini wachezaji  watano kati ya 11 wa Simba watakaoishukia Yanga Jumapili ijayo ni wapya kabisa.
Wachezaji hao walioko kwenye kambi ya Simba, Kigamboni, Dar es Salaam ni kipa Abel Dhaira na beki Joseph Owino ambao ni raia wa Uganda, Warundi Gilbert Kaze na Amisi Tambwe na mshambuliaji wa Tanzania, Betram Mwombeki.
Dhaira, Owino, Tambwe, Kaze na Mwombeki ni miongoni mwa wachezaji wapya waliosajiliwa na Simba na ambao wamejihakikishia namba kwenye timu hiyo inayofundishwa na Kocha Abdalah Kibadeni na msaidizi wake, Jamhuri Kihwelo.
Mbali na wachezaji hao wanaofanya vizuri, kikosi cha Simba kitawakosa wachezaji sita waliocheza pambano la mzunguko pili msimu uliopita dhidi ya Yanga lililopigwa Mei 18 na Yanga kushinda 2-0.
Wachezaji hao ni kipa Juma Kaseja, mshambuliaji Felix Sunzu, mabeki Shomari Kapombe, Mussa Mude na viungo Mrisho Ngasa na Mwinyi Kazimoto.
Wakati Kaseja na Sunzu mikataba yao ilimalizika, Mude alikatishwa mkataba, Kapombe alitimkia Ufaransa kufanya majaribio ya soka la kulipwa kama ilivyo kwa Kazimoto aliyekwenda nchini Qatar, huku Mrisho Ngasa akihamia Yanga.
Hata hivyo,Yanga inayonolewa na kocha wake yule yule Mdachi Ernest Brandts inatarajia kushuka uwanjani na wachezaji 10 kati ya 11 waliocheza mechi dhidi ya Simba Mei 18 huku Simba pia ikiwa imemtimua kocha wake wa kipindi hicho, Patrick Liewig raia wa Ufaransa.
Mchezaji pekee kwenye kikosi cha Yanga ambaye atacheza mchezo huo kwa mara ya kwanza tangu aliposajiliwa ni Ngassa mwenye mabao mawili miongoni mwa vinara wa kutikisa nyavu katika Ligi Kuu msimu huu.
Katika hatua nyingine, Owino amesema kuwa: “Kwa upande wetu tuko vizuri, mimi na mwenzangu, Kaze hakuna shida tumekamilika, lakini mechi yetu na Yanga kulingana na uzoefu wangu wa miaka mingi ina changamoto nyingi.”
“Nimewaona Yanga wanavyocheza ukilinganisha na sisi tunavyocheza nashindwa hata kutabiri naona atakayelala vizuri na kuamka na bahati atashinda, tunatakiwa kucheza vizuri, kuhakikisha tunafunga mabao mapema ili kucheza kwa nafasi,”alisema.
Mechi ya Simba na Yanga huwa na ushindani mkubwa kutokana na upinzani wa miaka mingi wa timu hizo na katika maandalizi yao, Simba wamejificha ufukwe wa Bamba na Yanga wapo Pemba.
CHANZO: MWANASPOTI

Share story hii kupitia>>>>>> :
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

Category:

0 comments