MAJANGA MAN U
BEKI Patrice Evra amesema kwamba ataondoka Manchester United mwishoni mwa msimu.
Beki
huyo wa kushoto wa Ufaransa aliulizwa kuhusu Mkataba wake ambao
unamalizika Juni na kama ataongeza na majibu yake yalikuwa anataka
kuondoka Old Trafford.
Evra
ameumizwa na kuondoka kwa Sir Alex Ferguson aliyestaafu na
hajapendezewa na mpango wa klabu hiyo kutaka kuwasajili Leighton Baines
na Fabio Coentrao.
Alisema:
"Hapana, hapana kabisa. Ni mambo binafsi. Si kwamba Manchester United
haitaki mimi nisaini mkataba mpya. Hii kwa ujumla na mambo binafsi.
Manchester United wandependa mimi nimalizie soka yangu huko, lakini hiki
ni kitu fulani binafsi,".
Mtendaji
Mkuu wa United, Ed Woodward amewaambia mashabiki kwamba Baines alikuwa
mlegwa wa awali wa klabu, lakini Everton ilitaka dau kubwa kumuuza.
Evra
amekuwa akihusishwa na mpango wa kurejea kwao Ufaransa kujiunga na
klabu yake ya zamani, Monaco na matajiri wa nchini humo, Paris
Saint-Germain kwa miezi kadhaa.
Mlengwa: Manchester United walitaka kumsajili Leighton Baines ambaye anaweza kumpindua Evra kikosi cha kwanza
Pigo: Evra pia hakufurahishwa na kuondoka kwa kocha gwiji wa klabu hiyo, Sir Alex Ferguson
Evra pia anakabiliwa na moto mwingine kutokana na kuwashambulia kwa maneno wachambuzi wa soka wa nchini mwake.
Ametakiwa
na Shirikisho la Soka Ufaransa kufafanua madai yake, ambayo
yamemhusisha pia mshindi wa Kombe la Dunia mwaka 1998, Bixente Lizarazu
na wachambuzi wengine watatu kwenye TV.
Category: uingereza
0 comments