KUELEKEA BRAZIL 2014: HATIMA YA UFARANSA, HISPANIA, ENGLAND KUJULIKANA LEO
Tayari makundi ya A, B, C, D, na E yalishapata vinara
watakaoiwakilisha Ulaya nchini Brazil, ambapo nchi za Ubelgiji, Italia,
Ujerumani, Uholanzi na Uswisi zimefuzu fainali hizo, huku makundi ya F, G, H na
I yakitarajia kupata vinara wake leo
KINYANG’ANYIRO cha kuwania tiketi ya kufuzu Kombe la Dunia
mwakani nchini Brazil, Kanda ya Ulaya kinaendelea leo kwa miamba minne kusakwa
kukamilisha idadi ya timu za bara hizo, baada ya nyingine tano kujikatia tiketi
zake.
Tayari makundi ya A, B, C, D, na E yalishapata vinara
watakaoiwakilisha Ulaya nchini Brazil, ambapo nchi za Ubelgiji, Italia,
Ujerumani, Uholanzi na Uswisi zimefuzu fainali hizo, huku makundi ya F, G, H na
I yakitarajia kupata vinara wake leo.
Shughuli pevu leo inayakabili mataifa ya Ufaransa, Hispania,
England, Ugiriki, Ureno na Russia, zitakazoshuka kwenye viwanja mbalimbali
kuwania pointi muhimu, huku nyingine zikiombea mabaya kwa wapinzani kuweza
kujihakikishia tiketi ya Brazil.
Mabingwa watetezi, Hispania na kikosi kinachonolewa na Fabio
Capello cha Russia, vitakuwa na kibarua kipevu cha kuzipiku Ufaransa na Ureno
katika jaribio la kufuzu fainali za mwakani, ingawa miamba itakayozidiwa kete
hapo itakuwa na mechi za mtoano wa ‘best-losers.’
Mechi za mtoano ‘best losers play-off’ utajumuiosha timu nane
zenye matokeo bora kutoka katika makundi yote, ili kupata timu nne
zitakaoungana na vinara tisa kufanya jumla ya timu 13 za bara la Ulaya
zitakazofuzu Brazil 2014.
Hispania inaingia dimba la nyumbani kusaka sare dhidi ya Georgia
ili kufuzu fainali za mwakani, bila kujali matokeo ya Ufaransa itakayokuwa
nyumbani kuikaribisha Finland, kama ilivyo pia kwa Russia, inayohitaji pointi
pia dhidi ya Azerbaijan kuitibulia Ureno.
Russia inaizidi Ureno pointi tatu, hivyo ukiondoa sare
kuweza kufuzu Brazil, itahitaji maombi ili Ureno ipoteze nyumbani dhidi ya Luxemburgo,
matokeo yatakayoiacha juu ya kilele cha kundi F la michuano hii ya awali.
Katika kundi H, England na Ukraine zote zina nafasi ya
kufuzu fainali zijazo, ambapo ‘Three Lions’ wanaongoza kwa pointi 19, moja juu
ya Ukraine, ambapo kila moja inaiombea mabaya yenzake huku ikihitaji ushindi
kujihakikishia tiketi ya moja kwa moja.
England watakuwa nyumbani Wembley kuwaalika Poland ambao
wanakamilisha ratiba, huku Ukraine wao wakiwa ugenini kuwavaa wenyeji wao San
Marino – ambao wana rekodi chafu ya kufungwa mechi zote tisa za kundi hilo,
ikiburuza mkia bila pointi.
Katika kundi la G, Bosnia-Herzegovina wanaongoza kwa tofauti
ya mabao juu ya Ugiriki, kila moja ikiwa na pointi 22, hivyo mechi zao leo ni
za kufa na kupona katika jaribio la kufuzu kwa fainali za mwakani.
Wakati vinara Bosnia-Herzegovina watakuwa ugenini kuwavaa
Lithuania, wapinzani wao Ugiriki watakuwa nyumbani kuwaalika ‘vibonde’
Liechtenstein, ambao wanabuiruza mkia wa kundi G wakiwa na pointi mbili baada
ya mechi zao tisa.
Jijini London, England wanaingia dimbani wakiwa na
kumbukumbu ya sare ya bao 1-1 dhidi ya Poland kwenye dimba la Wembley,
iliyowanyima tiketi ya kufzu fainali za Kombe la Dunia la mwaka 1974.
Licha ya rekodi hiyo, kocha wa England, Roy Hodgson meonesha
shaka ya kuwashinda Poland, hasa kutokana na ushindani na wakati mgumu
waliowapa katika mechi ya kwanza baina ya nchi hizo iliyopigwa jijini Warsaw.
"Niliwaona wao katika mechi ya kichapo cha bao 1-0 kutoka
kwa Ukraine Ijumaa). Katika kipindi cha kwanza walicheza vvizuri sana, wakiwa
na nafasi nyingi za kufunga mabao,” alisema Hodgson.
"Kama wao watacheza vizuri kesho Jumanne (leo) dhidi
yetu, kama walivyocheza kipindi cha kwanza dhidi ya Ukraine, basi mechi yetu
itakuwa ngumu.
"Lakini daima mimi nimekuwa nikiwaunga mkono wachezaji.
Nawaamini wao, hasa ukizingatia sisi ndio pekee ambao hatujafungwa mechi katika
kundi letu.
"Tuna uwezo wa kuendeleza kutofungwa kwetu katiika
mechi ya 10, na ukizingatia tutakuwa na nafasi ya kupewa sapoti na mashabiki
wetu tutakapocheza Wembley, nitawasapoti wao. Nitakuwa mjinga kutowapa nguvu
nyota wangu," alisisitiza Hodgson.
RATIBA YA MECHI ZA LEO KOMBE LA DUNIA - BARANI ULAYA
Cyprus v Albania
Ugiriki v Liechtenstein
Lithuania v Bosnia-Herzegovina
Azerbaijan v Russia
Israel v Ireland Kask.
Ureno v Luxembourg
Norway v Iceland
Uswisi v Slovenia
Hungary v Andorra
Romania v Estonia
Uturuki v Uholanzi
Latvia v Slovakia
Bulgaria v Jamh. Czech
Denmark v Malta
Serbia v Macedonia
Jamh. Ireland v Kazakhstan
Sweden v Ujerumani
Vis. Faroe v Austria
Italia v Armenia
Ufaransa v Finland
Hispania v Georgia
San Marino v Ukraine
Montenegro v Moldova
England v Poland
Ubelgiji v Wales
Scotland v Croatia
BBC/Supersport.com
Category: uingereza
0 comments