Kavumbagu, Kaze ndani ya bifu zito

Unknown | 9:34 AM | 0 comments

 


Didier Kavumbagu.
Wilbert Molandi na Lucy Mgina
MSHAMBULIAJI wa Burundi, Didier Kavumbagu, amesema kuwa akiwa ndani ya uwanja katika mechi ya Ligi Kuu Bara keshokutwa Jumapili, ataweka undugu pembeni na beki wa kati wa Simba, Kaze Gilbert ambaye ni Mrundi mwenzake.
Kaze Gilbert.
Wachezaji hao wanaotoka nchi moja ya Burundi na waliowahi kucheza katika timu ya Vital’O inayoshiriki Ligi Kuu ya Burundi, watakutana uso kwa uso kwa mara ya kwanza tangu waanze kuzitumikia klabu zao za hapa nchini.
Akizungumza na Championi Ijumaa, Kavumbagu alisema kuwa siku hiyo atakuwa kazini, hivyo suala la kuwa wametoka nchi moja ataliweka pembeni kwa muda.
“Mimi na Kaze ni kama ndugu kutokana na wote kutoka nchi moja, pia tumetoka wote kwenye klabu moja ya Vital’O ya Burundi, lakini katika mechi ya Simba na Yanga, undugu nitauweka pembeni.
“Yeye kama beki atafanya kazi yake ya kuzuia na mimi nitafanya kazi yangu ya kufunga,” alisema Kavumbagu.

Share story hii kupitia>>>>>> :
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

Category:

0 comments