JANUZAJ AAMUA KUBAKI MAN UNITED, ASEMA ANATAKA KUWA MCHEZAJI BORA WA DUNIA
KINDA Adnan Januzaj amesema kwamba anataka kuongeza Mkataba kuendelea kucheza Manchester United.
Kijana
huyo mwenye umri wa miaka 18, alifunga mabao mawili dhidi ya Sunderland
katika mchezo wake wa kwanza wa Ligi Kuu England kwa mabingwa hao
watetezi na anatarajiwa kusaini Mkataba wa muda mrefu Old Trafford.
Mkataba
wa sasa wa Januzaj unatarajiwa kumalizika Juni 2014 na vigogo wa Ulaya,
Juventus na Barcelona wanataka saini ya kiungo huyo, lakini anatarajiwa
kubaki United na kusaini Mkataba mpya.
Atachezea nchi gani?
KOSOVO: Asili ya baba yake, Abedin, aliyezaliwa Kosovo. Lakini Kosovo si mwanachama wa FIFA.
UBELGIJI: Alipozaliwa. Alizaliwa mjini Brussels na kuishi huko hadi alipotimkia Manchester.
ALBANIA: Ni kwa asili. Wazazi wake asili yao Albanian.
UTURUKI: Kwa ukoo. Babu zake ni Waturiki.
ENGLAND: Mhamiaji, ikiwa ataishi England kwa miaka mingine mitano atapewa uraia.
"Nina
furaha Manchester United na ninataka kujifunga kwa asilimia 100 kufanya
vizuri katika kila mechi," Januzaj aliiambia Shirika Televisheni ya
Kosovo, KTV.
"Nataka kuisaidia Manchester United kushinda ubinga wa Ligi Kuu na kuwa mchezaji bora duniani,".
Mustakabali
wa soka ya kimataifa bado haueleweki kwa Januzaj, pamoja na hayo kinda
huyo haruhusiwi kuichezea England hadi awe ameishi kwa miaka mitano
nchini humo.
Amekwishaishi England kwa miaka miwili, hivyo atalazimika kusubiri hadi mwaka 2016.
"Ni baba yangu anayemua nichezee timu gani ya taifa, nitachezea atakapoamua, hivyo nitamsikiliza yeye,"alisema Januzaj.
Anataka kuwa matawi ya juu: Januzaj amesema anataka kuwa mchezaji bora duniani
Mkali wa maba: Januzaj aliifungia mabao mawili United dhidi ya Sunderland
Anabaki: Januzaj anatarajiwa kubaki Manchester United
Category: uingereza
0 comments