Glovu za Abel Dhaira zarudishwa kwa uongozi Simba SC
Kipa wa Simba, Abel Dhaira.
Na Khatimu NahekaKOCHA wa makipa wa Simba, James Kisaka, amemuweka chini kipa wake namba moja, Abel Dhaira ili wazungumzie tatizo alilonalo na kutema mipira, lakini kipa huyo akaibua siri moja kubwa inayosababisha tatizo hilo.
Kisaka amesema alilazimika kuzungumza na kipa huyo, ambapo Dhaira ametaja sababu kubwa ni glovu anazodakia.
“Ameniambia kuwa tatizo kubwa ni glovu anazotumia ambazo hazina ubora unaotakiwa,” alisema Kisaka na kuongeza:
“Dhaira amesema glovu ambazo anatumia katika mazoezi wakati mwingine ndiyo hizo anazotumia katika mechi, kitu ambacho siyo sahihi, lakini nimemweleza anatakiwa kuondoa hali hiyo na hilo la glovu nitaliwasilisha kwa viongozi ili walishughulikie haraka.”
Matukio ya kutema mipira mchezoni yamesababisha kuwe na hofu kubwa kutoka kwa mashabiki wa timu hiyo kwa kuwa hata katika mechi iliyopita dhidi ya Tanzania Prisons alifanya hivyo zaidi ya mara moja.
Category: tanzania
0 comments