MOYES ALIVYOBADILI KIKOSI MAN UNITED...AMA KWELI HIZI NI ZAMA MPYA OLD TRAFFORD
PICHA ya mbele ya kikosi cha Manchester
United imebadilika kwa mara ya kwanza baada ya miaka 27 huku David Moyes
akitokea katikati mbele yangu Sir Alex Ferguson astaafu.
Picha mpya imetolewa kwenye ukurasa wa
Twitter klabu, na Moyes akiwa amepo katikati ya Nahodha wake, Nemanja
Vidic na kiungo mkongwe, Ryan Giggs.
Picha hiyo pia inamhusisha mchezaji
mpya, Marouane Fellaini, ambaye amepozi katikati kwa mstari wa mwsiho
kabisa, na Wayne Rooney, ambaye alivumishwa kutaka kuondoka klabu hiyo
majira ya joto, amepozi mbele kulia. Taji la Ligi Kuu ya England na Ngao
ya Jamii pia yamo pichani.
Kikosi kipya: Manchester United imetoa
picha mpya kwa ili ya msimu mpya na David Moyes, Marouane Fellaini na
Wilfried Zaha ni miongoni mwa waliomo
KIKOSI CHA MANCHESTER UNITED 2013-2014
Kikosi cha Manchester United(Nyuma kabisa kutoka kushoto:) Danny Welbeck, Phil Jones, Chris Smalling, Jonny Evans, Marouane Fellaini, Rio Ferdinand, Michael Carrick, Robin van Persie
(Katikati kutoka kushoro:) Ofisa
Garry Armer, Mchambuzi wa viwango vya mchezo, Paul Brand, Mkuu wa
Ufiti, Tony Strudwick, Antonio Valencia, Darren Fletcher, Wilfried Zaha,
Adnan Januzaj, Fabio da Silva, Ofisa Rod Thornley, Mtunza Vifaa, Alec
Wylie, Physio Neil Hough
(Mstari wa pili kutoka kushoto:) Mtunza
vifaa Msaidizi, Ian Buckingham, Daktari Rob Swire, Dk Steve McNally,
Alexander Buttner, Sam Johnstone, Anders Lindegaard, David de Gea, Ben
Amos, Ashley Young, kocha Phil Neville, Ofisa Andy Caveney, kocha wa
makipa, Chris Woods.
(Mbele kutoka kushoto:) Shinji
Kagawa, Rafael da Silva, Anderson, Nani, Assistant Manager Steve Round,
Ryan Giggs, Kocha David Moyes, Nemanja Vidic, Kocha Jimmy Lumsden,
Patrice Evra, Javier "Chicharito" Hernandez, Tom Cleverley na Wayne
Rooney
Mataji matatu: Sir Alex Ferguson, Roy Keane na wakiwa na mataji matatu ambayo klabu ilishinda msimu wa 1999-2000
Mabingwa wa Ulaya: Matt Busby, Bobby
Charlton na George Best katika kikosi kilichotwaa ubingwa wa Ulaya kwa
kuifunga Benfica mwaka 1968
Mitambo ya umeme: Ron Atkinson na kikosi cha msimu wa 1982-1983 wakiwa na bidhaa za wadhamini wa wakati huo, Sharp
Wanatembea: Wachezaji wa Manchester United wakiondoka Uwanja wa Old Trafford baada ya kupiga picha ya timu
Anakosekana: Sir Alex Ferguson hayumo kwenye picha mpya baada ya kustaafu
Bao la mwisho kabla ya picha: Hernandez alifunga bao pekee United ikiifunga Liverpool katika Kombe la Ligi jana
Category: uingereza


0 comments