MANJI AKUTANA NA WACHEZAJI WA YANGA KIMYA KIMYA USIKU WA LEO ... HAYA NDIYO WALIYOTETA ...
| MANJI ALIPOKUWA AKIZUNGUMZA NA WACHEZAJI WA YANGA MSIMU ULIOPITA, LEO AMEKUTANA NA KIKOSI HICHO TENA KWENYE HOTELI YA SERENA JIJINI DAR |
Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji amekutana na wachezaji wa kikosi cha Yanga usiku huu.
Manji amekutana na wachezaji hao pamoja na benchi la ufundi ambalo limeongozwa na Kocha Mkuu, Ernie Brandts
Mkutano
huo wa kimyakimya ambao waandishi wa habari hawakutakiwa kuhudhuria
umefanyika kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Katika
mkutano huo, Manji amezungumza mambo mbalimbali na wachezaji hao ikiwa
ni pamoja na suala la kupoteza mchezo dhidi ya Azam FC.
Yanga iliyocheza vizuri katika mechi hiyo, ilipoteza kwa kuchapwa mabao 3-2.
“Lengo la mwenyekiti lilikuwa ni kuhakikisha tunaangalia wapi tumejikwaa na baada ya hapo tunaendelea mbele.
“Kikubwa
amesisitiza kuangalia zaidi ushirikiano na kwamba sisi ni mabingwa hivyo
lazima tupambane bila ya kujali timu zinatupania kupita kiasi,” alisema
mtoa habari.
Wachezaji takribani wote wa Yanga walihudhuria mkutano huo na baadaye walipata chakula cha usiku pamoja.
Category: tanzania


0 comments