HATIMAYE BINGWA WA DUNIA MKANDA WA (WBF) FRANCIS CHEKA ARUDI SHULE KUSOMA HUKO MJINI MOROGORO BAADA YA KUKOSA ELIMU YA SEKONDARI IKIWEMO NA KUPEWA CHEO CHA WAZIRI WA MICHEZO... CHEKI HAPA
Bingwa wa dunia mkanda wa WBF uzani wa Super Middle, Francis Cheka ‘SMG’ akiwaonyesha mashabiki mkanda wa ubingwa huo waliojit
okeza
kando ya barabara eneo la stendi kuu ya daladala wakati wa mapokezi
yake baada ya kumtwanga bondia Phil Williams wa Marekani jijini Dar es
Salaam hivi karibuni.
Na Juma Mtanda, Morogoro.
BINGWA
wa dunia wa mkanda wa ngumi wa WBF, Francis Cheka (SMG) anatarajiwa
kupewa cheo cha Waziri wa michezo katika chuo cha St Joseph School
Morogoro pindi atakapoanza rasmi masomo katika chuo hicho mkoani
Morogoro.
Mkuu
wa chuo cha St Joseph School Morogoro, Seif Chomoka kuwa Cheka atapewa
cheo cha uaziri wa michezo mara baada ya kuanza rasmi masomo yake ya
hesabu, masomo ya kingereza na kompyuta katika chuo chao kufuatia kupewa
ufadhili wa kusoma bure.
Chomoka
alisema kuwa licha ya Cheka kuwa bingwa wa dunia wana imani cheo cha
uaziri ndani ya chuo atautumia vyema katika kuandaa michezo mbalimbali
ikiwemo mchezo soka, ngumi, kukimbia na mingine.
“Cheka
tutampa cheo cha uaziri wa michezo pindi atakapoanza rasmi masomo yake
ya hesabu, masomo ya kingereza na kompyuta katika chuo chao kufuatia
kupewa ufadhili wa kusoma bure na tunaamini wanafunzi wenzake
watajifunza mambo mengi kutoka kwake”. Alisema Chomoka.
Cheka
amepewa fursa ya kusoma ndani ya chuo kwa sababu ya mchango wake wa
kuiletea sifa njema Tanzania na kuitangaza ramani ya mkoa wa Morogoro
ndani na nje ya dunia, vinginevyo fursa hiyo asingeweza kupata kutokana
na sifa za chuo hicho kinachomtaka mwanachuo kuwa na sifa ya kuwa na
elimu ya kidato cha nne na kuenelea. Alisema Chomoka.
Chomoka
alisema kuwa Cheka ameandaliwa programu maalum kujifunza masomo hayo
kwa hatua za awali kisha januari mwaka 2014 ataanza masomo ya kozi ya
information technolog kwa ngazi ya cheti na stahashada ambapo baada ya
kumaliza kozi hiyo itamsaidia kutumia vyema elimu hiyo fursa ya
kujitanga kimataifa kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii.
Naye
mwalimu aliyekabidhiwa jukumu la kumfundisha Francis Cheka, James Mkisi
alisema kuwa Cheka alitarajiwa kuanza masomo yake leo (jana) kwa masomo
ya hesabu na kingereza huku ratiba ikionyesha kuanza majira ya saa 4
hadi saa 5 asubuhi.
Mkisi
alisema kuwa ratiba ya bondia huyo imepangwa kulinagana na muda wake
kwa hawakutaka kuvuruga ratiba ya mazoezi yake ya mchezo wa ngumi na
itahusisha masomo ya komputa na hesabu likiwemo la introduction to
computer kwa siku ya jumanne kuanzia saa 3:00 hadi saa 4:00 asubuhi na
kingereza wakati siku ya jumatano ni kingereza na introduction to
computer kuanzia saa 5:00 asubuhi hadi 6:00 mchana.
Siku
ya jumatano atasoma kingereza na introduction to computer saa 5:00
asubuhi hadi saa 6:00 mchana na saa 6:00 hadi saa 7 mchana huku siku ya
alhamisi ikionyesha kusoma saa 4 hadi 5 asubuhi na saa 6:00 mchana hadi
saa 7:00 hadi saa 8:00 wakati ijumaa ambapo masomo hayo atasoma kwa muda
wa miezi mitatu huku mwalimu huyu akiamini tayari Cheka atakuwa amepata
mwanga kwa ajili ya kuanza rasmi somo kozi ya information technolog kwa
ngazi ya cheti na stahashada januari 2014.
Mkisi
alisema kuwa kwa upande wa kozi ya kompyuta yatahusisha kozi ya
introductioni computer, Microsoft word, Microsoft excel, Microsoft
access, Microsoft power point, Microsoft publishe na internet
application. CHANZO JUMAMTANDA.BLOGSPOT.COM
Category: tanzania


0 comments