AVB NA MOURINHO WAINGIA KATIKA VITA YA MANENO, WAPIGANA VIJEMBE VYA NGUVU!!

Unknown | 9:58 PM | 0 comments

 

Na Baraka Mpenja kwa msaada wa Sportsmail
HOMA ya pambano kali hapo kesho ligi kuu soka nchini England baina ya Tottenham Hospurs dhidi ya Chelsea, zote za London katika dimba la White Hart Lane inazidi kupamba moto, huku makocha wa timu hizo wakitupiana maneno ya kejeli kati yao na kikubwa ni kukosoana aina ya mpira unaochezwa na timu zao.
Kocha wa Chelsea, Mreno, Mario Jose Dos Santos Ferlix Mourinho amemtuhumu waziwazi kocha wa Tottenham Hospurs,  Andre Villas-Boas kuwa aache tabia ya kitoto baada ya kuanza vita ya maneno, lakini amekiri kuwa Spurs msimu huu ni washindani wa kweli wa kombe la ligi kuu soka nchini England.
Mournho amejibu maneno ya Villas-Boas aliyekaririwa akisema kuwa kamwe hapati usingizi kutokana na matatizo yao makubwa waliyoyapata msimu uliopita, hivyo lazima msimu huu afanye kazi na kuwapiku wenzake katika mbio za kuwania ubingwa akiwemo kocha wa Chelsea..
Mourinho alisema: ‘Mimi sio mtoto – kama nina tatizo na mtu yeyote namfuata tunazungumza na kuyamaliza”
Jose Mourinho
Anahofu? Jose Mourinho amekiri kuwa Totenham watatoa changamoto kubwa ya ubingwa msimu huu
Jose Mourinho
Kitu cha London: Jose Mourinho akiangalia mazoezi ya vijana wake kuelekea mchezo wa kesho dhidi ya Spurs 
 
chelsea trainingMourinho aliuliza uhusiano wa Andre Villas-Boas’s na Sir Bobby Robson.

Robson anasemekana aliingia katika mahusiano yasiyo mazuri na  AVB baada ya kocha huyo kumuingilia katika masuala ua upangaji wa timu katika klabu ya Porto.
Lakini, alipoulizwa kama mambo ya Robson yatakuwa na ushawishi katika mchezo wa kesho katika dimba la White Hart Lane, Mourinho alisema: ‘Wapi Andre alifanya kazi na Bobby Robson? Niambieni – wapi, alifanya kazi naye?’
‘Namkumbuka mke wangu na watoto wangi kila wakati nikifika hapa asubuhi – hivyo ndivyo ilivyo.’
chelsea trainingWachezaji wenye ujuzi mkubwa: Oscar (katikati), Eden Hazard (kulia)  na Samuel Eto’o  wakiangaliwa na Mourinho
 
 
Jose MourinhoHakuna mapenzo tena: Jose Mourinho (kushoto) na Andre Villas-Boas wameingia katika vita ya maneno
 
Juan Mata Mata anaweza: Mourinho amekiri kuvutiwa na kiwango cha Mhisapania huyo katika mchezo wa Capital One Cup
Wakati huo huo , Mourinho anatarajia kumtumia Juan Mata katika dimba la White Hart Lane kesho baada ya kuonesha kiwango cha hali ya juu dhidi ya Swindon.
Kocha wa Chelsea aliongeza: ‘Ana akili za kitaalamu na kimataifa. Amefanya jitihada kubwa kunishawishi nimuamini. Kwahiyo sasa niko upande wake.’
RATIBA YA MECHI YA KESHO LIGI KUU SOKA NCHINI ENGLAND NI KAMA IFUATAVYO
England: Premier League
28/09 04:45
Tottenham
Chelsea
 
28/09 07:00
Manchester United
West Bromwich Albion
 
28/09 07:00
Southampton
Crystal Palace
 
28/09 07:00
Hull
West Ham
 
28/09 07:00
Fulham
Cardiff
 
28/09 07:00
Aston Villa
Manchester City
 
28/09 09:30
Swansea

Share story hii kupitia>>>>>> :
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

Category:

0 comments