Wakati zimebaki siku chache kukamilika kwa idadi ya timu zitakazoshiriki Kombe la Dunia nchini Russia, mpira utakaoutumika umejulikana.

Huu ni Telstar 18 evokes ambao ubunifu wake umetokana na ule mpira uliotumika katika Kombe la Dunia mwaka 1970.

Mpira huo aina ya Adidas, zaidi umeangaliwa ule waliotumia magwiji kama Pelé, Gerd Müller, Giacinto Facchetti, Pedro Rocha na Bobby Moore walioshiriki michuano ya mwaka 1970.
 England. Cristiano Ronaldo ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa dunia wa Fifa 2017 baada ya kuwapiku wachezaji Lionel Messi na Neymar katika kipengele hicho.

Tuzo hizo zimetolewa Oktoba 23 ambapo mchezaji huyo aliyeambatana na mpenzi wake na mwanae amewashukuru waliompigia kura kwa kuweza kushinda pamoja na mashabiki na wachezaji wenzake.

“Nashukuru wote mlionipigia kura kwa kunifanya nishinde tuzo hii,” amesema Ronaldo.

Mbali na tuzo hiyo Ronaldo ametajwa katika kikosi bora cha mwaka 2017 ambacho kimewajumuisha Messi na Neymar na nyota wengine akiwemo Sergio Ramos, Toni Kroos, Andres Iniesta, na Dani Alves.

Tuzo ya mchezaji bora wa kike wa Fifa 2017 ilienda kwa Lieke Martens ambaye hakuudhuria katika utoaji wa tuzo kutokana na kujiandaa na kujiandaa na mechi ya kufuzu kombe la dunia la wanawake.

Ukumbi ulilipuka kwa shangwe wakati linatangazwa goli bora la mwaka ‘Puskas’ ambapo katika magoli 10 bora mashabiki walisikika wakimtaja nyota wa Arsenal, Olivier Giroud ambaye alitangazwa kama mshindi.

Wengine walioshinda tuzo za Fifa 2017 ni Zinedine Zidane (Kocha bora kwa waume), Sarina Wiegman (kocha bora kwa wanawake) Gianluigi Buffon (Kipa bora), Mashabiki wa Celtic (Kikundi bora), Francis Kone (Mchezo wa kiungwana).
KYLE WALKER

HATUA ya Tottenham kukamilisha usajili wa beki Davinson Sanchez, kumemfanya mlinzi huyo kuwa ingizo jipya katika orodha ya mabeki 10 ghali zaidi duniani.

Sanchez amejiunga na Tottenham akitokea Ajax ya Uholanzi huku pia licha ya kuingia katika orodha ya mabeki 10 ghali zaidi duniani, ameweka rekodi ya kuwa mchezaji ghali zaidi kuwahi kununuliwa katika historia ya klabu hiyo.

Kadhalika, Sanchez, 21, ndiye mchezaji kinda zaidi katika orodha hii ya mabeki 10 ghali zaidi, ambao nane kati ya hao ni uhamisho unaozihusisha klabu za Premier League na wanne wao wakiihusisha Manchester City.

Pia kutua huko kwa Sanchez Spurs, kunafanya mabeki watano kati ya hao 10 ghali, usajili wao umefanyika majira haya ya joto, wakati huu dirisha hilo likiendelea barani Ulaya kabla ya kufungwa Alhamisi saa sita usiku wiki hii.

Hapa ni mabeki hao10 ghali zaidi na kiasi cha fedha kilichotumika kuwanunua, je wana thamani hiyo?...

BENJAMIN MENDY – Monaco kwenda Man City (pauni milioni 51.75)

Pep Guardiola alivunja rekodi wakati alipomsajili Mendy kutoka Monaco Julai 24, mwaka huu, beki huyo wa kushoto ambaye ndiye ghali zaidi Ulaya, haraka alipata mafanikio msimu wa 2016-17 kwa kutwaa ubingwa wa Ligue 1 na kufika nusu fainali ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya akiwa na klabu yake hiyo ya awali.

Kutua kwake ni moja ya mkakati wa kutaka kushangaza kwa beki ya Man City, ambao umeifanya kutumia pauni milioni 165 kwa kununua mabeki watatu na kipa Ederson.

DAVID LUIZ – Chelsea kwenda PSG, pauni milioni 50

Dau hilo la Mendy, limefunika pauni milioni 50 Paris Saint-Germain ilizolipa wakati ikimsajili beki huyo wa kimataifa wa Brazil, Luiz kutoka Chelsea mwaka 2014.

Luiz alitwaa ubingwa wa Ligue 1 kwa misimu yote aliyoichezea PSG na amefanya hivyo mara tatu mfululizo huku akirudi Chelsea kwa pauni milioni 34 katika uhamisho wa kushangaza Agosti 2016, na kutwaa medali kwa kushinda Premier League.

KYLE WALKER – Tottenham kwenda Man City, pauni milioni 50

Wakati Walker anajiunga na Spurs akitokea klabu ya nyumbani kwao Sheffield United kwa pauni milioni tano mwaka 2009, mambo machache yalidhaniwa ikiwa ni pamoja na siku moja anaweza kuwa mchezaji ghali zaidi England.

Majumuisho hayo yote yanamaanisha Walker – ambaye hajawahi kutwaa kombe lolote katika wasifu wake kisoka– ana ‘chata’ kubwa ya kuweza kuishi Uwanja wa Etihad.

JOHN STONES – Everton kwenda Man City, pauni milioni 47.5

City ilionyesha kuridhika kulipa kiasi hicho kikubwa kwa kipaji hiki cha England, wakati Stones akijiunga na klabu hiyo kutoka Everton mwaka jana.

Lakini Stones, 23, alikumbwa na wakati mgumu katika mwaka wa kwanza wa Guardiola kwenye kikosi hicho kwa kucheza chini ya kiwango, wakiruhusu mabao mengi huku wakimaliza nafasi ya tatu katika msimamo wa ligi. Hata hivyo, kwa uwezo wa Stones unaweza bado kumuona akiendeleza kipaji chake.

DAVINSON SANCHEZ – Ajax kwenda Tottenham, pauni milioni 36.6

Spurs ilisubiri kwa wiki kadhaa kukamilisha usajili wao wa kwanza majira haya ya joto, lakini ikafanya hivyo staili yake, kwa kuvunja rekodi ya usajili wao na kumleta Sanchez Kaskazini mwa London.

Beki huyo wa zamani wa Atletico Nacional, aliripotiwa kuwa katika rada za Barcelona wakati Ajax ikitinga hatua ya fainali ya michuano ya Europa League mwaka jana, lakini baada kupokea kichapo cha mabao 2-0 kutoka kwa Manchester United, Jose Mourinho alifichua hofu ya uwezo wa mchezaji huyo ya kuwa na mpira miguuni mwake.

LEONARDO BONUCCI – Juventus kwenda AC Milan, pauni milioni 35.2

Kocha wa Juve, Massimiliano Allegri, alimshuhudia Bonucci akiruhusiwa kujiunga na wapinzani wao wa Serie A, AC Milan, ambayo ilimwaga fedha za kutosha sokoni ili kuweza kurudi Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Bonucci alitwaa ubingwa wa Serie A mara sita akiwa Juventus, lakini mara mbili walipoteza mechi ya fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya. Kusajiliwa kwa beki huyo wa kimataifa wa Italia– aliyeripotiwa kuwindwa na Chelsea –kulifanya mapinduzi makubwa kwa Milan.

SHKODRAN MUSTAFI – Valencia kwenda Arsenal, pauni milioni 35

Arsenal kawaida haijulikani kwa kutumia kiasi kikubwa kununua, huku kocha Arsene Wenger akijulikana katika ulimwengu wa soka kwa ubahili, lakini alitoa pauni milioni na kumsajili Mustafi kutoka Valencia Agosti 2016.

Beki huyo wa kimataifa wa Ujerumani alikuwa kisiki katika msimu wake wa kwanza Uwanja wa Emirates, lakini 'Gunners' ilikosa tiketi ya kushiriki Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao kwa mara ya kwanza tangu 1997.

ANTONIO RUDIGER – Roma kwenda Chelsea, pauni milioni 34

Wakati nguli wa klabu, John Terry, akiwa ameondoka Stamford Bridge, Chelsea ilikuwa katika mahitaji ya kusaka beki mpya wa kumrithi na ilimgeukia mshiriki mwenza wa Mustafi kimataifa kikazi, Rudiger, ambaye alijiunga nayo akitokea Roma.

Rudiger, 24, alitua London akiwa ndiyo kwanza wa moto akitokea kuipa mafanikio Ujerumani kwa kuibebesha Kombe la Mabara.

THIAGO SILVA – Milan kwenda PSG, pauni milioni 33

Ingizo la pili la PSG ni nahodha wa klabu yao, Thiago Silva, kwani Mbrazil huyo amekuwa chanzo cha mafanikio makubwa tangu alipojiunga nayo mwaka 2012.

Ingawa PSG ilikuwa imesimamishwa na Monaco kwa kukomesha utawala wao wa Ligue 1 msimu uliopita, Silva (32), ameiwezesha kutwaa ubingwa wa Ligue 1 mara nne na mara tatu wa Coupes de France.

ELIAQUIM MANGALA – Porto kwenda Man City, pauni milioni 32

Anguko kubwa la ada ya uhamisho wakati Mangala akijiunga na City kwa pauni milioni 32 kutoka Porto, lilionekana kuongezeka vya kutosha baada ya kuruhusiwa kujiunga na Valencia kwa mkopo. Lakini nyaraka zilizovuja baadaye zilipendekeza gharama ya jumla ya Mangala iliongezeka hadi pauni milioni 42.

Mangala alitarajiwa kuruhusiwa kuondoka na kocha Pep Guardiola, amecheza mechi 48 Premier League.

(*Gharama hizi zimeripotiwa kwa muda mara baada ya usajili kukamilika.)


WAKATI jumla ya mabao 19 yamefungwa kwenye mechi za raundi ya kwanza ya ligi hiyo iliyoanza juzi na kuendelea jana, Yanga imeendeleza rekodi ya Ligi Kuu Bara baada ya kulazimisha sare dhidi ya vijana wa Suleiman Matola, Lipuli FC ya Iringa.

Tangu msimu wa 2010/11, haijawahi kutokea mechi za ufunguzi za ligi hiyo kuchezwa bila kuwapo na mechi hata moja yenye matokeo ya sare, jambo ambalo kama mechi hiyo ya jana timu mojawapo ingeshinda basi ingekuwa ni rekodi mpya.

Aidha, mabao 19 yaliyofungwa katika mechi za ufunguzi msimu huu yamevunja rekodi ya magoli yaliyofungwa katika mechi za ufunguzi msimu uliopita uliokuwa na mabao 12 kwenye mechi zake za raundi ya kwanza.

Idadi hiyo ya mabao imepatikana baada ya matokeo ya Simba kushinda 7-0 dhidi ya Ruvu Shooting, Mwadui kuifunga Singida United 2-1 na Prisons kuitandika Njombe Mji 2-1.

Matokeo mengine ni Azam kuifunga Ndanda bao 1-0, Mbeya City kushinda bao 1-0 dhidi ya Majimaji, Mbao kuichapa Kagera Sugar bao 1-0, Mtibwa kuifunga Stand United 1-0 kabla ya jana Yanga kulazimishwa sare ya bao moja kwa moja.

Katika mechi ya jana ambayo ilipigwa kwenye Uwanja wa Uhuru, Yanga ambao walikuwa wanatafuta ushindi hasa baada ya watani zao wa jadi, Simba kuanza kwa kishindo cha ushindi wa bao 7-0 dhidi ya Ruvu Shooting, jana walikosa maarifa ya kuipenya ngome ya Lipuli iliyokuwa chini ya Asante Kwasi, aliyejiunga na timu hiyo msimu huu akitokea Mbao FC.

Wageni, Lipuli ndio waliokuwa wa kwanza kupata bao katika dakika ya 44 kupitia kwa mshambuliaji wa zamani wa Azam FC na JKT Ruvu, Seif Abdallah, aliyepiga shuti upande wa kulia wa Uwanja lililoenda moja kwa moja nyavuni na kumshinda golikipa Youthi Rostand.

Bao hilo lilidumu kwa dakika moja tu kutokana na Thaban Kamusoko kuisawazishia timu yake kwa kichwa akiunganisha nyavuni mpira wa kona uliochongwa na Ibrahim Ajibu.

Baada ya bao hilo, liliwafanya wachezaji wa Lipuli kumzinga mwamuzi Hans Mabena kufuatia mpira uliopigwa na Kamusoko kugonga mwamba wa juu na kuangukia ndani huku wachezaji wakidhani mpira huo uliangukia nje ya goli.

Pamoja na Yanga kufanya mashambulizi mfululizo, Lipuli walikuwa imara na kufanikiwa kuwabana Yanga wasipate bao la pili.

Hata hivyo, Lipuli ilipata pigo baada ya beki wake Kwasi kupewa kadi ya pili ya njano iliyomfanya kutolewa kwa nyekundu zikiwa zimebaki dakika mbili mpira kumalizika.

Baada ya mpira kumalizika mashabiki wa Yanga walionekana kuwatolea maneno machafu wachezaji wa Lipuli huku wakiwatuhumu kwa vitendo vyao vya kujiangusha mwishoni mwa kipindi cha pili.

Katika mchezo huo kiungo wa Yanga, Kabamba Tshishimbi alishindwa kuonyesha makeke yake kama alivyofanya kwenye mchezo dhidi ya Simba baada ya kubanwa na viungo wa Lipuli Sahaban Zuberi na Mussa Nampaka.



Shirikisho la mpira wa miguu duniani (FIFA) limetangaza majina ya makocha kumi watakaowania tuzo ya kocha bora wa mwaka 2017.

Katika kinyang’anyiro cha kuwania tuzo makocha kutoka ligi kuu England (EPL) wameongoza kwa kutajwa kwa majina manne, Ligi kuu ya Hispania (La Liga) Hispania majina matatu, Ligi kuu Ujerumani (Bundesliga) imetoa majina mawili huku Ufaransa na Italia ikitoa jina moja moja.

1- Massimiliano Allegri-Juventus

2- Carlo Ancelotti-Bayern Munich

3- Antonio Conte-Chelsea

4- Luis Enrique-Hispania

5- Pep Guardiola-Manchester City

6- Leonardo Jardim-AS Monaco

7- Joachim Low-Ujerumani

8- José Mourinho-Manchester United

9- Mauricio Pochettino

10- Diego Simeone-Atletico Madrid

11– Tite-Brazil

12- Zinédine Zidane-Real Madrid

Upigaji kura unaanza Agosti 21 na kufungwa Septemba 7 mwaka huu, kura zitapigwa na Makocha wa timu za Taifa, Manahodha, baadhi ya Wawakilishi kutoka vyombo vya Habari mbalimbali vitakavyoteuliwa pamoja na Mashabiki kwa Mujibu wa FIFA.

Orodha ya timu 10 zenye thamani ya juu duniani:

1. Dallas Cowboys $4.2bn (£3.26bn) American football

2. New York Yankees $3.7bn (£2.87bn) baseball

3. Manchester United $3.69bn (£2.86bn) football

4. Barcelona $3.64bn (£2.82bn) football

5. Real Madrid $3.58bn (£2.78bn) football

6. New England Patriots $3.4bn (£2.64bn) American football

7. New York Knicks $3.3bn (£2.56bn) basketball

8. New York Giants $3.1bn (£2.4bn) American football

9. San Francisco 49ers $3bn (£2.33bn) American football

10. Los Angeles Lakers $3bn (£2.33bn) basketball

Yanga ambao ni mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara watani zao mabingwa wa Kombe la FA, Simba watakutana katika mechi ya kuwania Ngao ya Jamii itakayopigwa Agosti 23, mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, imeelezwa.

Mechi hiyo ya Ngao ya Jamii ni maalum kwa ajili ya ufunguzi wa msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara 2017/18, ambao unatarajiwa kuanza Agosti 26, mwaka huu kwenye viwanja saba hapa nchini.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Ofisa Habari na Mawasiliano wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Alfred Lucas, alisema pia timu hizo zitakutana katika mechi ya kwanza msimu ujao ifikapo Oktoba 14, mwaka huu ambayo Simba itakuwa mwenyeji na itakuwa ikishuka uwanjani na kumbukumbu ya ushindi wa mabao 2-1 iliyoupata mechi ya mwisho zilipokutana.

Lucas alisema katika mechi ya ufunguzi wa ligi hiyo, Simba itaanza kuwania ubingwa huo unaoshikiliwa na watani zao kwa kuwakaribisha Ruvu Shooting ya Pwani wakati Azam FC itaanzia ugenini kwenye Uwanja wa Nangwanda Mtwara kwa kuwavaa Ndanda FC wakati Mwadui FC itachuana na Singida United ambayo imepanda daraja msimu huu.

Alisema siku hiyo ya ufunguzi pia Mtibwa Sugar watawakaribisha Stand United kwenye Uwanja wa Manungu huku Kagera Sugar ikikutana na majirani zao Mbao FC mjini Bukoba, Njombe Mji wakiwasubiri Tanzania Prisons huku Majimaji ya Songea wakiwafuata Mbeya City jijini Mbeya.

Mabingwa watetezi, Yanga wenyewe wataanza kutetea ubingwa wao Agosti 27, mwaka huu kwa kuwakaribisha Lipuli FC ya Iringa ambayo sasa iko chini ya nahodha na kiungo wa zamani wa Simba, Selemani Matola.

“Maandalizi ya ligi hiyo yako katika hatua nzuri, lakini tunazikumbusha klabu kuwa hatutaruhusu makocha ambao hawana sifa kuendelea kuziongoza timu hizo kwa mujibu wa kanuni ya 11 ambayo inataka kocha wa timu ya Ligi Kuu kuwa na leseni ya kuanzia Daraja B huku [wanaozinoa] Daraja la Kwanza ikiwa ni kuanzia Daraja C,” alisema Lucas.

Aliongeza kuwa kabla ya kuanza kwa ligi hiyo kutakuwa na semina na mitihani ya majaribio kwa waamuzi na msimu huu mchakato huo utafanyika katika kituo kimoja cha Dar es Salaam kuanzia Julai 28 mpaka 31, mwaka huu.

Aidha, aliwakumbusha viongozi wa timu zote 16 zinazotarajiwa kushiriki ligi hiyo kukamilisha taratibu za usajili wa wachezaji ambao dirisha lake litafungwa rasmi ifikapo Agosti 6, mwaka huu.
REAL MADRID imesema inaweza kupokea Paundi milioni 350  ambazo ni sasa na Sh. Trilioni 1.3 ili kumruhusu mchezaji wao Cristiano Ronaldo kuondoka  klabuni hapo na kujiunga na klabu za Paris Saint-Germain au Manchester United.

Mchezaji mwenye umri wa miaka 32 hana furaha ya kuweko kwake na klabu hiyo ya Bernabeu kutokana na kutoungwa mkono katika mapambano yake na mamlaka za kodi za Hispania, pia kile anachoona kutotendewa haki na vyombo vya habari na kuzomewa kwa mara kwa mara ambako amekuwa akifanyiwa na mashabiki wa Real Madrid.

Hata hivyo, alisaini mkataba mpya wa miaka mitano na mabingwa hao mnamo Novemba mwaka jana ambapo mshahara wake kwa wiki ni Pauni 350,000, ambayo ni sawa na Sh. Bilioni 1.

Dau la kuuzwa kwake limepangwa kuwa ni Pauni 870, kiwango ambacho hakuna klabu yoyote inayoweza kulitoa, zikiwemo za China.  Hata hivyo, Rais wa Real Madrid, Florentino Perez, amesema klabu yake inaweza kuchukua Pauni milioni 350 ili kumuuza Ronaldo.
Baada ya msimu uliopita Chelsea kubeba taji la ligi kuu nchini Uingereza, leo ratiba mpya imetoka ya msimu ujao wa ligi huku Tottenham waliokuwa wapinzani wakubwa wa Chelsea msimu uliopita watakutana mwanzoni tu wa ligi.

2/08/2017 15:00 Chelsea v Burnley

19/08/2017 15:00 Tottenham Hotspur v Chelsea

26/08/2017 15:00 Chelsea v Everton

09/09/2017 15:00 Leicester City v Chelsea

16/09/2017 15:00 Chelsea v Arsenal

23/09/2017 15:00 Stoke City v Chelsea

30/09/2017 15:00 Chelsea v Manchester City

14/10/2017 15:00 Crystal Palace v Chelsea

21/10/2017 15:00 Chelsea v Watford

28/10/2017 15:00 Bournemouth v Chelsea

04/11/2017 15:00 Chelsea v Manchester United

18/11/2017 15:00 West Bromwich Albion v Chelsea

25/11/2017 15:00 Liverpool v Chelsea

29/11/2017 19:45 Chelsea v Swansea City

02/12/2017 15:00 Chelsea v Newcastle United

09/12/2017 15:00 West Ham United v Chelsea

12/12/2017 19:45 Huddersfield Town v Chelsea

16/12/2017 15:00 Chelsea v Southampton

23/12/2017 15:00 Everton v Chelsea

26/12/2017 15:00 Chelsea v Brighton and Hove Albion

30/12/2017 15:00 Chelsea v Stoke City

01/01/2018 15:00 Arsenal v Chelsea

13/01/2018 15:00 Chelsea v Leicester City

20/01/2018 15:00 Brighton and Hove Albion v Chelsea

31/01/2018 19:45 Chelsea v Bournemouth

03/02/2018 15:00 Watford v Chelsea

10/02/2018 15:00 Chelsea v West Bromwich Albion

24/02/2018 15:00 Manchester United v Chelsea

03/03/2018 15:00 Manchester City v Chelsea

10/03/2018 15:00 Chelsea v Crystal Palace

17/03/2018 15:00 Burnley v Chelsea

31/03/2018 15:00 Chelsea v Tottenham Hotspur

07/04/2018 15:00 Chelsea v West Ham United

14/04/2018 15:00 Southampton v Chelsea

21/04/2018 15:00 Chelsea v Huddersfield Town

28/04/2018 15:00 Swansea City v Chelsea

05/05/2018 15:00 Chelsea v Liverpool

13/05/2018 15:00 Newcastle United v Chelsea
Mashabiki wa Arsenal wamekosa raha kwani ubingwa wa ligi kuu Uingereza umekuwa mgumu sana kwao, baada ya Wenger kupewa mkataba mpya pengine katika msimu ujao wa ligi anaweza kuwapa kikombe, hii ndio ratiba ya Arsenal msimu ujao.



12/08/2017 Leicester City (h)

19/08/2017 Stoke City (a)

26/08/2017 Liverpool (a)

09/09/2017 Bournemouth (h)

16/09/2017 Chelsea (a)

23/09/2017 West Bromwich Albion (h)

30/09/2017 Brighton and Hove Albion (h)

14/10/2017 Watford (a)

21/10/2017 Everton (a)

28/10/2017 Swansea City (h)

04/11/2017 Manchester City (a)

18/11/2017 Tottenham Hotspur (h)

25/11/2017 Burnley (a)

28/11/2017 Huddersfield Town (h)

02/12/2017 Manchester United (h)

09/12/2017 Southampton (a)

12/12/2017 West Ham United (a)

16/12/2017 Newcastle United (h)

23/12/2017 Liverpool (h)

26/12/2017 Crystal Palace (a)

30/12/2017 West Bromwich Albion (a)

01/01/2018 Chelsea (h)

13/01/2018 Bournemouth (a)

20/01/2018 Crystal Palace (h)

30/01/2018 Swansea City (a)

03/02/2018 Everton (h)

10/02/2018 Tottenham Hotspur (a)

24/02/2018 Manchester City (h)

03/03/2018 Brighton and Hove Albion (a)

10/03/2018 Watford (h)

17/03/2018 Leicester City (a)

31/03/2018 Stoke City (h)

07/04/2018 Southampton (h)

14/04/2018 Newcastle United (a)

21/04/2018 West Ham United (h)

28/04/2018 Manchester United (a)

05/05/2018 Burnley (h)

13/05/2018 Huddersfield Town (a)