SIRI YA JEZI NAMBA 10 BARCELONA

Unknown | 4:09 PM | 0 comments


KILA timu kubwa duniani ina utamaduni wake wa kuthamini na kuzipa uzito wa juu namba za jezi, ambazo zimetumiwa na mastaa wake wa zamani.

Si kila mchezaji hupewa namba hizo pindi anaposajiliwa na mastaa wengi wamekuwa wakitoa masharti ya namba za jezi wanazotaka kuvaa.

Pale Manchester United kwa sasa kuna mgogoro wa chini kwa chini baada ya kinda wa Ufaransa, Anthony kuporwa jezi namba tisa na kukabidhiwa gwiji, Zlatan Ibrahimovic.

Katika kikosi cha Man United, jezi namba 7, 8,9, 10 na 11 zimekuwa moto kutokana na kutumiwa na magwiji na mastaa wakubwa duniani. Awali, namba 7 ilikuwa ikitumiwa na Eric Cantona kisha David Beckham na baadaye Cristiano Ronaldo, ambapo wote wameitendea haki vilivyo.

Kwa kikosi cha Barcelona, jezi namba 10 ambayo kwa sasa inatumiwa na staa wake, Lionel Messi, ndiyo kila kitu kikosini hapo na imebeba historia nzito.

Lakini si Messi tu ambaye ametumia jezi hiyo ambayo ina historia nzito kwa kuvaliwa na mastaa kutoka Amerika ya Kusini kikosini Barcelona na ambao, wameitendea haki vilivyo na kuifanya maarufu duniani.

Juan Roman Riquelme

Juan Roman Riquelme anatajwa kuwa mmoja wa wachezaji wa aina yake na waliojaaliwa kipaji kikubwa cha soka.

Staa huyo alisajiliwa na Barcelona kwa dau la pauni 11 milioni kutoka Boca Juniors ya Argentina, ambako alikuwa akipiga mpira mkubwa sana. Alipotua Camp Nou mwaka 2002 alikabidhiwa jezi namba 10, akibebeshwa jukumu zito na kuichezesha timu na kuipa mafanikio.

Hata hivyo, uhamisho wa Riquelme haukumfurahisha sana kocha Luis van Gaal, ambaye alikuwa akikinoa kikosi hicho akikosoa kuwa ulikuwa uhamisho wa kisiasa.

Kilichofuata ni van Gaal kukosa imani na Riquelme na katika kutimiza kauli yake hiyo alimchezesha winga badala ya kiungo mshambuliaji, ambako hata hivyo alipambana kuonyesha kiwango bora ili kumshawishi kocha huyo mdachi kumwamini.

Share story hii kupitia>>>>>> :
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

Category:

0 comments