Timu ya Copa Coca-Cola Tanzania yarejea nchini toka Afrika Kusini

Unknown | 11:37 PM | 0 comments


Timu ya Copa Coca-Cola iliyoshiriki katika michuano ya kimataifa ya Copa Coca-Cola nchini Afrika Kusini wiki iliyopita ikiwasili kwenye Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam  Jumatatu jioni. Timu hiyo ilitolewa katika hatua ya makundi na Zimbabwe kuibuka mabingwa.

Afisa maendeleo wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Salum Madadi akiipokea timu ya vijana ya Copa Coca-Cola iliyoshiriki katika michuano ya kimataifa ya Copa Coca-Cola nchini Afrika Kusini wiki  iliyopita. Timu hiyo ilitolewa katika hatua ya makundi na Zimbabwe kuibuka mabingwa.  Zimbabwe waliibuka mabingwa wa 2013 wa mashindano ya kimataifa ya COPA Coca-Cola kwa kuwafunga Uganda 3-0 katika mchezo wa fainali iliyochezwa High Performance Center, Pretoria, Afrika  Kusini.


Share story hii kupitia>>>>>> :
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

Category:

0 comments